*NI MAANDALIZI YA KUANZA ZIARA YA SIKU 22 KATIKA MIKOA YA RUVUMA NA MBEYA
*LEO ANAKUTANA NA WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM WILAYA YA MSASI.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasilimia baadhi ya viongozi wa CCM, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege mjini Mtwara asubuhi hii, tayari kwa safari ya kwenda katika mikoa ya Ruvuma na Mbeya kuanza ziara yake ya siku 22 katika mikoa hiyo kesho. Kabla ya kuwasili katika mikoa hiyo, akiwa mkoani Mtwara leo atakutana na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilayya Masasi.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, wakisalimiana na viongozi wa CCM baada ya kuwasili na Kinana mjini Mtwara asubuhi hii.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Kanali Joseph Simbakalia, Uwanja wa Ndege wa MtwaraKinana akiwa na viongozi wa mkoa wa Mtwara