Aliyekuwa Katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, Bryson Mwasimba akionbyesha kadi yake ya chama hicho, kabla ya kumkabishi Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto), alipotangaza kuhamia CCM, leo jioni katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika Kata ya Lupa, wilayani humo.
Bryson Mwasimba kutoka Chadema akikabishi kadi yake kwa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
"Sasa Nataka kuungama dhambi nilizowafanyia ndugu zanguni wakati nikiwa Chadema, Niliwadanganya mengi nanyi mkaniamini. Sasa naungama kwenu mnisamehe, Lakini mjue kwamba wenye lawama kubwa ni Chadema kwa sera zao za kuhimiza wanachama na viongozi wake kuwa waongo. Sasa kabla sijaendelea kusema yaliyo safi naomba kwanza nilivue gwanda hili la Chadema maana linaninajisi", alisema Bryson, akiwa jukwaani baada ya kutangaza kuhamia CCM kwenye mkutano huo.
"Sasa ngoja nilivulie mbali hili kwanda nibaki huru", akasema Bryson wakati akilivua gwanga lake la Chadema, huku akiwa ameshikilia mdomoni kadi yake mpya ya CCM aliyokabidhiwa na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kushoto).
Baada ya kulkivua gwanda, Bryson akavaa shati la kijani la CCM.
Kisha akazungumza ya moyoni, huku akimtwisha mzigo wa Lawama Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu, kwamba amekuwa akimtumbukiza kwenye madeni mbalimbali kwa kutumia huduma kisha kusepa bila kulipa. Wakati akisema hayo Nape alikuwa upande wa kulia akimtazama na kumsikiliza kwa makini sana
Ikawa nderemo na hoi hoi Bryson akabebwa na wana CCM kwa furaha
KABLA YA HAPO KINANA ALIKAGUA UJENZI BARABARA YA MBEYA-CHUNYA HADI TABORA INAYOJENGWA NA KAMPUNI YA CCCC YA CHINA
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na wasaidizi wake, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakikagua sehemu ya ujenzi wa barabara ya Mbeya-Chunya inayoenda hadi Tabora, unaofanywa na Kampuni ya Kichina ya CCCC, wakati Kinana na msafara wake walipokuwa wakipita katika eneo hilo, akiwa njiani kwenda wilayani Chunya, leo
Baadhi ya maeneo yanajengwa kwa uhodari mkubwa kiasi kwamba kupita ni lazima kuruka, Hapa Katibu wa NEC, Itukadi na Uenezi akiruka kutoka upande mmoja kwenda mwingine wa eneo hilo linalojengwa.Nyuma yake ni Kinana ambaye naye alimfuata Nape pia kwa kuruka eneo hilo
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akiruka eneo hilo
Kazi ya kuopasuka milima na kuweka sawa inapopita barabara hiyo, ikiendelea
MIKUTANO NA SHUGHULI NYINGINE ZA KINANA WILAYANI CHUNYA
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Katibu wa NEC, Itukadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwaslimia wananchi, baada ya msafara wa Kinana kuwasili wilayani Chunya
Kinana akiwasalimia wananchi baada ya kusimamia msafara wake akiwa njiani kwenda Chunya
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua shina la wakereketwa wajasiriamali wa CCM katika kituo cha mabasi mjini Chunya.
Kisha akakabidhi kazi za CCM kwa wanachama wapya 100 kwenye shina hilo
Kinana akihutubia baada ya kizindua shina hilo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsikiliza Kijana, Frank Mwapololo, ambaye ni mmoja wa wachimbaji wadogo katika machimbo ya mafunzo kwa ajili ya wachimbaji wadogo, yaliyopo Chunya, alipozungumza na wajasiriamali wa mradi huo, Nov 30, 2013, akiwa katika ziara kukagua utekelezaji wa ilani ya chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia sahihi ya kuzitatua, mkoani Mbeya.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (wapili kulia) akimrekebishia sawasawa vazi, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, baada ya wazee wa Kata ya Lupa, wilayani Chunya, kumvalisha vazi la wazee wa Kata hiyo, akiwa katika ziara kukagua utekelezaji wa ilani ya chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia sahihi ya kuzitatua, mkoani Mbeya
Katibu Mkuu wa CCM akiwahutubia wananchi wa Kata ya Lupa,
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi mashine isiyotumia umeme, ya kufyatulia matofali, kwa kikundi cha wajasiamali, wakati wa mkutano wa hadhara aliofanya Nov 30, 2013, katika Kata ya Lupa, wilayani Chunya, akiwa katika ziara kukagua utekelezaji wa ilani ya chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia sahihi ya kuzitatua, mkoani Mbeya, Nov 30, 2013. Wengine ni Mkuu wa mkoa huo, Abbas Kandoro na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye. Imatayarishwa na theNkoromo Blog
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
-
▼
2013
(633)
-
▼
November
(42)
- ZIARA YA KINANA WILAYANI CHUNYA MOTO, AMZOA KATIBU...
- MKUTANO WA KINANA TUNDUMA WAFUNIKA, MAELFU WAJITOK...
- KINANA NA MSAFARA WAKE WATINGA WILAYANI MOMBA LEO ...
- DUNIA MZOBORA KUZIKWA MCHANA HUU MAKABURI YA KISUT...
- WAKULIMA WA ILEJE WAIKATAA MBOLEA YA MINJINGU
- KINANA AWEKA HISTORIA YA KIPEKEE KATIKA ZIARA YAKE...
- WATENDAJI WATAKIWA KUTUMIKIA WANANCHI
- ZIARA YA KINANA YATIKISA KYELA, MAELFU WAFURIKA MI...
- KINANA AWASILI KYELA BAADA YA SAFARI YA ZAIDI YA S...
- KINANA AMALIZA ZIARA WILAYANI NYASA, AKWEA MELI KW...
- KINANA AVUNA WANACHAMA KIBAO KUTOKA UPINZANI
- KINANA AANZA ZIARA YA NYASA
- KINANA AZUNGUMZIA VIONGOZI WASIO NA SIFA
- KINANA: CCM HAITORUBUNIWA KWA AJILI YA KUPATA KURA
- WATENDAJI WA SERIKALI WATAKIWA KUWASIKILIZA WANANCHI
- WANACHAMA 300 KUTOKA UPINZANI WAJIUNGA NA CCM PERA...
- KINANA AAHIDI UTUMISHI ULIOTUKUKA
- KINANA AKUTANA NA WANA VYUO SONGEA MJINI
- MAELFU WAFURIKA MKUTANO WA KINANA SONGEA JIONI HII
- KINANA AWASILI WILAYA YA SONGEA MJINI
- KINANA NA UJUMBE WAKE WATINGA NAMTUMBO KIAINA, WAP...
- KINANA AMALIZA ZIARA YAKE WILAYA YA TUNDURU KWA MA...
- KINANA AHUTUBIA VIJIJI VITATU TUNDURU KUSINI
- WANANCHI KUSINI WATAKA KOROSHO IBANGULIWE NCHINI
- KINANA AWASILI TANDAHIMBA NA MASASI
- KINANA AWASILI MTWARA, YUPO NA DK. ASHA-ROSE MIGIR...
- DK. SENGONDO MVUNGI AMEFARIKI DUNIA LEO
- CCM: ZIARA ZA KINANA MIKOANI ZAONYESHA TIJA
- RAIS KIKWETE AMPA RUNGU MAGUFU7LI
- WAWEKEZAJI WA KUTOKA UBELGIJI WAWASILI NCHINI
- NAPE AWAKUNA WANANCHI WA TARIME, WASEMA SI MNAFIKI
- HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS ...
- DK. SENGONDO MVUNGI APELEKWA AFRIKA KUSINI LEO
- NSSF YAWASILISHA BUNGENI MPANGOKAZI WAKE WA UTEKEL...
- PRESIDENT KIKWETE ATTENDS AU SUMMIT IN PRETORIA
- WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA BUNGENI LEO
- WENYEVITI WA CCM KATA ZOTE WILAYANI KINONDONI, DAR...
- DK. REHEMA NCHIMBI: WENYEVITI CCM FANYENI KAZI YA ...
- NAPE ATIMIZA AHADI NYAMONGO
- WATANZANIA UINGEREZA WALIVYOMUAGA KWA WINGI RAIS J...
- RAIS KIKWETE KATIKA MKUTANO MJINI LONDON
- CCM NA CPC WAPEANA SOMO DAR
-
▼
November
(42)
LOVE LINKS
Powered by Blogger.