Google PlusRSS FeedEmail

KINANA AWASILI KYELA BAADA YA SAFARI YA ZAIDI YA SAA 24 KWA MELI KUTOKA MBAMBA BAY MKOANI RUVUMA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi, baada ya kuwasili katika bandari ndogo ya Kiwira, wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov 24,2013.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana 'akiwasaluti' Wananchi baada ya kuwasili katika bandari ya Kiwira, wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov 24, 2013. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Maganga Sengerema na kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiri (kulia), wakishuka kutoka katika mv Songea, baada ya msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kuwasili katika bandari ndogo ya Kiwira, wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov 24, 2013.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Godfrey Zambi, baada ya kushuka katika Mv Songea, baada ya kuwasili katika bandari ndogo ya Kiwira, wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov 24, 2013.
 Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe akimlaki wa furaha, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipompokea katibu mkuu huyo, baada ya kuwasili katika bandari ndogo ya Kiwira, wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov 24, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwapungia mkono wananchi, baada ya kuwasili katika bandari ndogo ya Kiwira, wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov 24,2013.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (Kushoto, aliyenyoosha mkono) akikagua kivuko katika bandari ya zamani ya Itunge, baada ya kuwasili  wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov 24, 2013. Bandari hiyo ambayo imekufa kwa miaka mingi sasa, ipo katika mpango wa kufufuliwa na serikali.
 Nahodha wa mv Songea Tom Faya akimpatia maelekezo ya namna meli hiyo inavyofanya kazi, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake, wakati katibu mkuu huyo alipokuwa  akisafiri na meli hiyo kutoka Mbamba Bay mkoani Ruvuma kwenda Kyela mkoani Mbeya, leo Nov 24,2013. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Siasa na Uhisiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro. Kwenye usukukani ni Nahodha Msaidizi, Conrad Shauritanga.
Baadhi ya abiria waliosafiri na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana katika mv Songea, alipokuwa alitokea Mbamba Bay mkoani Ruvuma kwenda Kyela mkoani Mbeya. Meli hiyo iliyoanza kazi katika Ziwa Nyasa, mwaka 1974, ina uwezo wa kubeba abiria 213 wakiwemo wafanyakazi 13 wa meli hiyo.

This entry was posted in

One Response so far.

  1. Kazi nzuri Nkoromo Unavyojua angle za Photoooo hadi raha, Niimani yangu sasa chama Kimerudi kwenye heshma yake.

Leave a Reply