Google PlusRSS FeedEmail

ZIARA YA KINANA JIMBO LA SONGWE WILAYANI CHUNYA YAFANA, AFUNGUA NA KUSHIRIKI UJENZI WA MIRADI YA MAENDELEO

 KATIBU Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana akishiriki na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kati) na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha_rose Migiro, katika ujenzi soko la Kata ya Mwambani, Makongolosi, Chunya, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadili nao njia ya kuzitatua, mkoani Mbeya
 Nape na Dk Asha -Asha-Rose wakishuka baada ya kushiriki ujenzi soko la Kata ya Mwambani, Makongolosi, Chunya
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kulia) akikagua bweni la wasichana, shule ya sekondari Maweni, Kata ya Mwambani, Chunya, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadili nao njia ya kuzitatua, mkoani MbeyaDes Mosi, 2013. Wapili kushoto ni Mkuu wa shule hiyo Elly Mnyalape.
 Dk Asha-Rose  akiwa na wnafunzi wa kike shule ya sekondari Maweni, , Mwambani, Chunya
 Kinana akifunga skrubu wakati akiweka mlango kwenye nyumba ya walimu na watumishi wa hospitali, Saza, Chunya. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, wakishiriki ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya sekondari Kapalala, wilayani Chunya.
 HUMU YAMO MAJI KWELI? Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisikiliza kama tanki lina maji alipozindua mradi wa maji safi na salama katika Kijiji cha wafugaji cha Mteka, wilayani Chunya
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Gegwa Luhende baada ya kuzindua mradi wa maji safi na salama katika kijiji cha wafugaji wa Kisukuma cha Mteka, Chunya
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakilachakula cha asili ya jamii ya wafugaji wa Kisukuma, katika msitu wa kijiji cha wafugaji hao cha Mteka, Chunya
 Kinana akikagua lambo la kunyweshea mifugo katika kijiji cha wafugaji cha Mteka, Chunya
MTUMBIWI HUU UTATUMIA KUCHOTEA WANACHAMA: Katibu Mkuu wa CCM Abdul;rahman  Kinana akiwa na zawadiza mtumbwi aliopewa na wazee katika kijiji cha Udinde, Chunya
 HATA ALA HII YA MUZIKI NAJUA KUITUMIA: Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kuungurumisha ngoma inayotumbuizwa kwa mtungi na kigoda, iliyokuwa ikipigwa na kina mama katika kijiji cha Udinde, Chunya
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano Udinde, Chunya
 Wananchi kwenye mkutano wa Kinana, Udinde: Imetayarishwa na theNkoromo Blog

This entry was posted in

Leave a Reply