Google PlusRSS FeedEmail

RAIS KIKWETE AMTEUA DK. ASHA-ROSE MIGIRO KUWA MBUNGE, KINANA, NAPE NA KANDORO WAMPONGEZA WAKIWA MBEYA

Dk. Asha-Rose Migiro
DAR ES SALAAM, Tanzania
Rais, Dk. Jakaya Kikwete amemteua Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Maifa (UN) Mstaafu, Dk. Asha-Rose Migiro kuwa Mbunge.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jijini Dar es Salaam, imesema, Uteuzi huo ambao umetangazwa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, ulianza tangu jana, Dese,mba 2, 2013.


Dk. Asha-Rose Migiro kwa sasa ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, anayesimamia Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI).


Akizungumzia uteuzi huo, mjini Mbalizi jioni hii,  akiwa Mbalizi mkoani Mbeya, Dk. Asha-Rose amemshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa uteuzi, akisema  ameupokea kwa furaha, na kueleza kuwa kitendo hicho kinadhihirisha jinsi Rais Kikwete alivyo na imani naye pamoja na imani kwa Wanawake wa Tanzania
PONGEZI ...
 Kufuatia uteuzi huo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpongeza Dk.Asha-Rose Migiro leo jioni, mjini Mbalizi mkoani Mbeya ambako wapo katika ziara ya kukagua utekeleza wa ilani ya CCM, na kusikiliza kero za wananchi kwa lengo la kuzipatia ufumbuzi
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimpongeza kwa uteuzi huo wa Rais Kikwete
 Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akimpongeza Dk. Asha-Rose Migiro kwa uteuzi huo wa Rais
.Dk. Asha Rose Migiro akizungumza na waandishi wa habari waliomfuata kutaka kujua ameupokeaje uteuzi huo wa Rais Kikwete. Nape, Kandoro na Dk. Asha-Rose mwenyewe wapo Mbalizi, katika ziara ya Kinana kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua. Picha kwa hisani ya Kamanda wa Matukio Blog

This entry was posted in

Leave a Reply