KAMPUNI ya Smart Banking Solutions (SBS) imezindua kadi mpya ya huduma za kifedha inazowezesha watu wa viwango mbalimbali vya kipato kupata huduma bora kwa haraka na kisasa zaidi kupitia benki.
Uzinduzi wa kadi hiyo umefanyika wiki hii jijini Dar es Salaam, kwa kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Jaji Mstaafu Thomas Mihayo ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa B-PESA Gustav Vermaas, alisema, kadi hiyo ni ya malipo ya kabla, ambapo mmiliki wa kadi ya aina anaweza kutumia kiasi cha fedha ambacho tayari amekiingiza na kukitunza katika kadi yake husika.
"Kadi hii inaruhusu kuwa na matumizi mengi pamoja na kuhamisha fedha kwenye kadi na kulipia ankara au bili, kununua bidhaa na kulipia huduma", alisema.
Alisema, hapa Tanzania kumekuwa na matumizi machache ya huduma za kibenki katika jamii kutokana na watu wengi kukosa fursa ya kuingia katika mfumo rasmi wa kibenki.
Vermaas alisema kufuatia kuzinduliwa kwa kadi hizo, kutawezeshan hata watu weneye kipato cha chini kutunza fedha zao kwa urahisi na kujiwekea akiba kwa kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima.
Alifafanua kwamba sasa wananchi wanaweza kupata kadi za B-PESA kutoka sehemu yoyote aliyopo wakala wa huduma hiyo na kwenye benki ambazo ni wanachama wa huduma hiyo.
Kwa upande wake, mgeni rasmi Jaji Mstaafu Thomas Mihayo alisema, kupatikana kwa kadi za B-PESA kutasaidia kupounguza watu kutembea na fedha nyingi mifukoni kwa ajili ya kufanya manunuzi.
Alitoa mwito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kuitumia huduma hiyo ya B-PESA ili kujiweka salama wao na fedha zao kwa kuwa mbali na kuibiwa pia fedha ni kivutio cha majambazi ambao wengi wao hudhuru maisha kabla ya kupora.
Mwenyekiti wa Smart Banking Solutions (SBS), Edmund Mndolwa (kulia) akishangilia wakati Mkurugenzi Mtendaji wa SBC, Gustav Vermaasa alipokuwa akifungua rasmi kadi ya B-PESA wakati wa uzinduzi wa kadi hiyo juzi jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Jamji Mstaafu Thomas Mihayo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, pia akishangilia.
Mwenyekiti wa Smart Banking Solutions (SBS), Edmund Mndolwa (kushoto) Mkuu wa Kitengo cha ukuzaji Biashara, Elibariki Lukumay (wapili) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo na Mkurugenzi Mtendaji wa SBC Gustav Vermaasa wakikata keki maalum iliyonakshiwa alama za kadi ya B-PESA, wakati wa uzinduzi wa kadi hiyo ya B-PESA juzi jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Smart Banking Solutions (SBS), Edmund Mndolwa (kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa B-PESA Gustav Vermaasa wakati wa uzinduzi wa kadi ya B-PESA juzi jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wakurugenzi na Maofisa wa B-PESA wakiwa kwenye uzinduzi huo
ITM zinazotumiwa na kadi za B-PESA zikionyeshwa kwenye uzinduzi huo. Kadi hizo zinazotumia 'cheap card' zinaingia kwenye ITM yoyote.
Kadi za B-PESA kwa huduma mbalimbali. |