Google PlusRSS FeedEmail

KINANA AMALIZA ZIARA MBEYA VIJIJINI, ATINGA MBEYA MJINI LEO ASUBUHI, AZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI WA TAZARA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Maombi, Kata ya Mbalizi, Mbeya Vijijini, jana, Des 3, 2013, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua mkoani Mbeya.
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mbeya mjini, Ephraim Mwaitenda akiwatambulisha viongozi wake kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, katika mapokezi kuingia mbeya mjini
 Vijana wakiwa na mabango wakati wa mapokezi ya Kinana kutoka Mbeya Vijijini kuingia Mbeya mjini leo asubuhi
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA Richard Festo, alipowasili leo kwenye stesheni ya Reli hiyo mjini Mbeya, kuzungumza na wafanyakazi wa shirika hilo la reli, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua mkoani Mbeya.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA), leo Des 4, 2013, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua mkoani Mbeya. Wengine kutoka kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Mbunge Mteule, Dk. Asha-Rose Migiro na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na Mbunge wa Mbozi Mashariki Godfrey Zambi.
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Mbunge Mteule, Dk. Asha-Rose Migiro akiwasalimia wafanyakazi wa TARAZA kwenye mkutano huo na Kinana
 Mwenyekiti wa Wafanyakazi wa TAZARA Ally Mkami akisoma risala ya wafanyakazi
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwasalimia wafanayakazi wa TAZARA
 Wafanyakazi wa TAZARA wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipozungumza nao leo mjini Mbeya
 Katibu wa NEC, Itikasi na Uenezi, Nape Nnauye akiwa ameketi kwenye mkeka na wananchi wengine, wakati wa kikao cha shina kilichofanyika  nyumbani kwa mjumbe wa shina namba 14, mjini Mbeya leo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpa kadi mmoja wa wanachama wapya Elizabeth Mwakalebela, wakati wa kikao kilichofanyika nyumbanbi kwa mjumbe wa shina namba 14, na kuhudhuriwa na Kinana, mjini Mbeya leo
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Mbunge mteule, Dk. Asha-Rose Migiro (kushoto) akiwa ameketi kweneye mkeka  na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mbeya Dk. Mary Mwanjelwa, katika kikao kilichofanyika nyumbani kwa mjumbe wa shina namba 14, Mbeya Mjini.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza kwenye kikao kilichofanbyika nyumbani kwa mjumbe wa shina namba 14, Mbeya mjini leo.

This entry was posted in

Leave a Reply