SHUNYANGA, Tanzania
Diwani wa CCM katika kata ya Mwakitolyo, katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Kasanga Lumala (75) amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu kifua kikuu.
Taarifa iliyopatikana kutoka mjini Shinyanga, imesema, diiwani huyo alifariki jana mida ya saa 10 jioni katika hospitali ya mkoa alikokuwa amelazwa kwa muda wa siku mbili baada ya kuzidiwa akiwa nyumbani wakati akiendelea kutumia dawa .
Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Ngassa Sosthenes amesema hayo, akizungumza na waandishi wa habari mjini Shinyanga na kufafanua kwamba katika uhai wake diwani huyo alisumbuliwa na maradhi ya ugonjwa huo wa kifua kikuu licha ya kwamba alikuwa akipata katika hospitali mbalimbali.
Alisema, Desemba 26 mwaha huu, walipata taarifa ya kuzidiwa kwa diwani huyo wakaamua kumpeleka haraka katika hospitali hiyo kwa kushirikiana na ndugu zake na madaktari kuendelea kumfanyia uchunguzi zaidi.
Amesema leo mwili umetolewa hospitali na kuumpeleka kwenye kata yake kwa ajili ya wananchi kwenda kutoa heshima za mwisho kabla ya mazishi kwenda kufanyika mkoani Geita katika kata ya Mlele walikozikwa pia wazazi wake.
Kwa mujibu wa Kaim Kwenyekiti huyo wa Halmashauri, Diwani huyo aliyezaliwa mwaka 1937, ameacha watoto saba wajane wawili na amekuwa diwani wa kata hiyo kwa awamu mbili mfululizo tangu mwaka 2005.
Msiba wa diwani huyo umekuja huku msiba mwingine wa Diwani wa kata ya Nyida ukiwa bado unaombolezwa na wananchi kufuatia diwani nao Mshindikwa Masele (40) kufariki dunia kutokana na ajali ya pikipiki yake aliyokuwa akiiendesha akitokea Isaka wilayani Kahama Desemba 21, mwaka huu.