DAR ES SALAAM, Tanzania
KADI za B-PESA zilizozinduliwa mapema wiki hii, zimeelewa kuwa usalama wake wa fedha za mteja ni wa hali ya juu.
Imeelezwa kwamba wakati uwezekano ni mkubwa kuhamisha taarifa kwa njia ya ki-eletroniki kutoka katika kadi zinazotumia teknolojia ya 'magnetic' ni vigumu kufanya hivyo kwenye kadi ya B-PESA ambazo teknolojia yake ni ya 'cheap' kama ile ya kwenye laini za simu za mkononi.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam, na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Smart Banking Solutions (SBS) iliyozindua huduma za kadi hizo za B-PESA, Gustav Vermaas, mapema wiki hii.
Amesema watumiaji wa kadi hizo ambazo zina huduma mbalimbali ikiwemo kuhifadhi fedha, watakuwa na uhakika wa usalama wa fedha zao hata kama wataibiwa au kupoteza kadi.
Vermaas alisema, ikitokea kuibiwa au kupotea kwa kadi, mteja atatakiwa kuikumbuka tu namba ya siri ya kadi yake ambayo itarahisisha kutengenezewa nyingine itakayomuwezesha kuendelea na matumizi huku fedha zake zikiwa salama.
Alisema kadi hiyo imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa, hivyo hakuna haja ya wananchi kuogopa kuitumia kwani ni sawa na kutembea na benki.
“Unapokuwa na kadi hii, unakuwa unatembea na fedha zako, hivyo unapokuwa na shida, unaingia kwenye mashine zilizoingia ubia na benki au mawakala kutoa fedha au kulipia huduma mbalimbali bila matatizo yoyote, ”alisema.
Alisema kwamba, watumiaji wataweza kutumia mashine za ATM za benki mbalimbali zilizoingia ubia, ingawa kutakuwepo mawakala maeneo mbalimbali kwa ajili ya kupata hudama ya B-PESA.
Aidha, alisema B-PESA itatoa huduma kwa kushirikiana na wadau tofauti zikiwemo benki na mawakala kwa lengo la kurahisisha matumizi ya fedha.
“Mtu anayetaka kusajili kadi ya B-PESA, anatakiwa kwenda kwa wakala aliye karibu huku akiwa na simu ya mkononi. Baada ya kumaliza kujisajili atapokea ujumbe mfupi kwenye simu yake ambao utathibitisha usajili na namba yake ya siri,”alifafanua.
Alifafanua kuwa, matumizi ya kadi ya B-PESA hayana tofauti na zile za ATM za benki zingine, kwani nazo mtumiaji wake atatakiwa kuingiza kadi yake kwenye mashine za B-PESA, hivyo kutakiwa kuhakikisha kiasi unachotaka kulipa au kutoa na kutakiwa kuingiza namba za siri.
“Baada ya kumaliza kuingiza namba ya siri utapata stakabadhi na lazima uhakikishe kuwa stakabadhi ni sahihi na uitunze. Pia, unaweza kujiunga na mtandao wetu wa kutuma taarifa kwenye simu kila ufanyapo muamala,”alifafanua.
Kadi ya B-PESA inaruhusu kuwa na matumizi mengi ikiwemo uhamisho wa fedha kwenye kadi, kutolea fedha, kuingiza fedha, na kulipia bili,kununua bidhaa na kulipa huduma mbalimbali.
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
-
▼
2013
(633)
-
▼
December
(66)
- CCM BLOG YAWATAKIA HERI NA FANAKA WADAU WOTE KATIK...
- SALAMU ZA MWAKA MPYA ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGAN...
- KUELEKEA KATIBA MPYA: TASISI ZA KIJAMII, VYAMA VY...
- AMIRIJESHI MKUU, RAIS JAKAYA KIKWETE AMWAPISHA MKU...
- MZEE MWINYI AFUNGUA MAKAO MAKUU YA BPZ MJINI ZANZIBAR
- RAIS KIKWETE AMTEUA ERNEST MANGU KUWA MKUU MPYA WA...
- CCM YAIPONGEZA TUME YA KATIBA
- RAIS KIKWETE, DK. SHEIN WAKABIDHIWA RASIMU YA PILI...
- PATA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO
- KAMPUNI YA UJENZI WA BARABARA YA GNSM CONTRACORS C...
- DIWANI MWINGINE WA CCM AFARIKI DUNIA SHINYANGA
- SEMVUA: KASI YA MTEMVU INAENDANA NA YA KINANA, NAPE
- RAIS KIKWETE AWAJULIA HALI WAGONJWA WALIOLAZWA MUH...
- RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI AKITOKEA MAREKANI KUCHE...
- JAJI WARIOBA KUKABIDHI RASIMU KWA RAIS KIKWETE, DK...
- WAJUKUU WAMUUA BABU YAO KWA KIPIGO SIKU YA KRISMAS...
- MSIKILIZE LIVE, DAKTARI HUYU WA KUTIBU UMASIKINI
- KIONGOZI ADAIWA KUINGIA MITINI TEMEKE, ASAKWA NA W...
- RAIS KIKWETE AENDELEA VEMA NA UCHUNGUZI WA AFYA YA...
- X-MASS NJEMA KWA WOTE
- PINDA APOKEA MSAADA WA PIKIPIKI 44
- WATENGENEZAJI SABA WA MAMBOMU YA KIVITA WASHIKWA K...
- EWURA YATANGAZA BEI MPYA YA UMEME
- DIWANI WA CCM AFARIKI KWA AJALI YA PIKIPIKI YAKE S...
- CHOLAGE AFUNGA SEMINA YA UVCCM MABIBO, AKABIDHIWA ...
- VIJANA WAMPONGEZA RAIS KIKWETE KUWAWAJIBISHA MAWAZ...
- DR SHEIN, SADIFAH WAFUNGUA MATEMBEZI YA VIJANA KUA...
- KUTANA NA STEVEN MHINA DUNGUMALO WA UHURU FM
- NAPE: NI SAHIHI MAWAZIRI KUWAJIBISHWA
- MWALIKO KWA MAKUNDI MBALIMBALI KUPENDEKEZA MAJINA ...
- DK. FENELLA AFUNGA SEMINA YA WAZAZI WILAYA YA KINO...
- SEMINA YA VIONGOZI WA JUMUIA YA WAZAZI YA CCM WIL...
- NDEGE YA ETHIOPIAN AIRLINE YANUSURIKA AJALI YATUA ...
- CCM MOROGORO WAFAGILIA ZIARA ZA KINANA MIKOANI, NI...
- SABA MBARONI KWA MAUAJI YA MWENYEKITI WA ZAMANI WA...
- BABA NA BINTIYE WAFA KWA KUPIGWA NA RADI GEITA
- MKE WA RAIS, MAMA SALMA KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO ...
- JUMUIA YA WAZAZI YA CCM KINONDONI WAENDA KUJINOA M...
- UNIC YAFANYA MAFUNZO YENYE TIJA YA UJASIRIMALI PEMBA
- BAADA YA KUZINDULIWA KADI ZA B-PESA SASA KAMPUNI Y...
- MWENYEKITI WA ZAMANI WA CCM MKOA WA MWANZA AUAWA N...
- JK ATUNUKU KAMISHENI JWTZ
- HOTUBA YA RAIS KIKWETE KWENYE MAZISHI YA MANDELA
- KAMATI KUU YA CCM YAWAHOJI MAWAZIRI SABA, MMOJA BA...
- WATEJA WA KADI ZA B-PESA WAHAKIKISHIWA USALAMA WA ...
- LOWASSA ANUSURIKA KIFO KATIKA AJALI YA NDEGE ARUSHA
- HUDUMA MPYA YA KADI ZA B-PESA YAZINDULIWA TANZANIA
- MTEMVU AZIDI KUWAPATIA WATANZANIA KAZI DUBAI
- DK.ASHA-ROSE MIGIRO AAPISHWA BUNGENI LEO
- MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA RASMI MAKTABA YA SHULE ...
- MAMASALMA AMPOKEA MALKIA MAXIMA WA UHOLANZI NA BAA...
- TAMKO LA WENYEVITI WA CCM-MIKOA LA KUMPONGEZA KATI...
- RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAELFU YA WANANCHI MAA...
- SAFARI YA KINANA KUTOKA MAKAMBAKO- DAR ES SALAAM
- WAANDISHI WALIOSAFIRI KATIKA ZIARA YA KATIBU MKUU ...
- KINANA AKABIDHI KADI UVCCM 120 NJOMBE, AZINDUA ALB...
- MAPOKEZI MAKUBWA YAMSUBIRI KINANA DAR ES SALAAM, ...
- KINANA AKUTANA NA WANAFUNZI WA VYUO ELIMU YA JUU W...
- KINANA ACHAPA KAZI LEO WANGING'OMBE, NJOMBE
- KINANA AINGIA MAKETE, AKABIDHI TREKTA KWA USHIRIKA...
- CCM YAITEKA MBEYA MJINI JIONI YA LEO, KINANA ASAFI...
- KINANA AMALIZA ZIARA MBEYA VIJIJINI, ATINGA MBEYA ...
- RAIS KIKWETE AMTEUA DK. ASHA-ROSE MIGIRO KUWA MBUN...
- KINANA AWASILI MBEYA VIJIJINI MCHANA HUU
- KINANA AITEKA MBARALI, RUJEWA YARINDIMA, MAELFU YA...
- ZIARA YA KINANA JIMBO LA SONGWE WILAYANI CHUNYA YA...
-
▼
December
(66)
LOVE LINKS
Powered by Blogger.