Hapa ndiyo mpakani mwa Mbeya na Makete, ni eneo la Mfumbe ndiko Katubu Mkuu wa CCM Abdulrahmam Kinana na msafdara wake wamepokelewa na viongozi wa mkoa wa Njombe na kuagwa na wale wa mkoa wa Mbeya
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abas Kandoro baada ya kufika kwenye mpaka huo. Wapili kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Maganga Sengerema
Kinana akiwa na Kandoto (kulia) na Mkuu wa mkoa wa Njombe Kanali mstaafu Aseri Msangi kwenye mpaka huo |
Kinana akipita katika paredi la Vijana wa CCM Makete akivuka mpaka kutoka Mbeya kwenda Mkoani Njombe. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Katibu Mkuu wa CCM (aliyevaa fulana nyeusi ya CCM-kulia), akishiriki kucheza ngoma ya bakora, katika kijiji cha Ndananga, Makete mkoani Njombe
Mkurugenzi wa mawasiliano CCM, Daniel Chongolo akipata mlo kiana msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana ulipofika katika kijiji cha Ndananga, Makete mkoani Njombe
Huu ndiyo mji wa Njombe katika baadhi ya maeneo yake |
KINANA AKABIDHI TREKA
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akilima kwa trekta kwenye shamba ya Ushirika wa Vijana wa Kata ya Ndananga, wilayani Makete, kabla ya kukabidhi trekta hilo kwa uongozi wa vijana hao, jana, Des 5, 2013. Trekta hilo limetolewa na CCM kufuatia ahadi aliyoitoa Katibu Mkuu huyo, alipotembelea Kata hiyo mwanzoni mwa mwaka huu. Mradi huo wa shamba la ushirika wa vijana lina jumla ya hekta 300.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akilima kwa trekta kwenye shamba ya Ushirika wa Vijana wa Kata ya Ndananga, wilayani Makete, kabla ya kukabidhi trekta hilo kwa uongozi wa vijana hao, jana, Des 5, 2013. Trekta hilo limetolewa na CCM kufuatia ahadi aliyoitoa Katibu Mkuu huyo, alipotembelea Kata hiyo mwanzoni mwa mwaka huu. Mradi huo wa shamba la ushirika wa vijana lina jumla ya hekta 300.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akishuka kwenye trekta baada ya kulima kwenye kwa trekta hilo kwenye shamba ya Ushirika wa Vijana wa Kata ya Ndananga, wilayani Makete, kabla ya kukabidhi trekta hilo kwa uongozi wa vijana hao, jana, Des 5, 2013. Trekta hilo limetolewa na CCM kufuatia ahadi aliyoitoa Katibu Mkuu huyo, alipotembelea Kata hiyo mwanzoni mwa mwaka huu. Mradi huo wa shamba la ushirika wa vijana lina jumla ya hekta 300. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi ufunguo wa trekta kwa Mwenyekiti wa Ushirika wa Vijana wa Kata ya Ndananga, wilayani Makete,Tunsome Shemngogo, jana, Des 5, 2013, kwa ajili ya mradi wa Ushirika huo wenye shamba la hekta 300 katika kijiji cha Mlengu kwenye kata hiyo. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kushoto) akiwa karibu na kijana, Josephat Ngogo aliyevaa kofia ya CHADEMA, wakati wa hafla ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kukabidhi trekta kwa Uhsirika wa Vijana wa Kata ya Ndananga, iliyofanyika jana Des 5, 2013, katika kijiji cha Mlengu wilayani Makete. Akikabidhi trekta hiyo ambayo CCM imetoa kufuatia ahadi yake alipotembelea Kata hiyo mwanzoni mwa mwaka huu, Kinana alisema, ni kwa ajili ya kusaidia Vijana wote bila kujali itikadi za vyama vyao.
KINANA ATEMBELEA VETA
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akitazama mfano wa ujenzi wa nyumba ya kisasa kwa matofali yasiyohitaji kutumia saruji wakati wa ujenzi, alipotembelea karakana ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) wilayani Makete, jana, Des 5, 2013. Wapili kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhisiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe, Deo sanga aka ah People.Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipata melezo kwenye maabara ya kupima viwango vya ubora wa udongo wa ufyatuaji matofali alipotembelea VETA. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Mbunge Mteule Dk. Asha-Rose Migiro
Kinana akijaribu shati aliloshonewa kwenye kituo hicho cha VETA. Kushoto ni Dk. Asha-Rose Migiro naye akiwa na zawadi yake ya nguo aliyopewa na mafundi cherehani wa kituo hicho.
Nape (kulia) naye pia akivaa shati lake aliloshonewa na VETA kwa vipimo vilivochukuliwa kwa kuona picha yake kulingana na maelezo ya mafunzi hao
Kinana akionyeshwa mashine ya kukereza mbao kwenye karakana ya kituo hicho cha VETA
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akijaribu moja ya cherehani za kuishonea nguo, alipofika kwenye karakana ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Makete, akiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Des 5, 2013.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akipanda mti wa kumbukumbu, alipotembelea Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Makete, jana Des 5, 2013. Kushoto ni Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Monica Mbele.
Dk. Asha-Rose Migiro akipozi picha na Mkurugenzi wa VETA Nyanda za Juu Kusini, Monica Mbele na Mkuu wa Wilaya ya Makete Josephine Matiro
Dk. Asha-Rose Migiro akimsahuri jambo Monica Mbele
Kinana na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi na watumishi wa VETA Makete
Wasanii wa kikundi cha VETA Makete wakiselebuka kufurahia ujio wa Kinana na ujumbe wake kwenye chuo hicho. Imetayarishwa na theNkoromo Blog