Google PlusRSS FeedEmail

WAJUKUU WAMUUA BABU YAO KWA KIPIGO SIKU YA KRISMAS!!!!

TABOTA, Tanzania 
Watu wawili wamekamatwa na Polisi wilaya ya Igunga mkoani Tabora kwa tuhuma za mauaji ya babu yao.

Watuhumiwa hao ni Mwashi Mipawa (17) na Kashinje Mipawa(15)wote wakazi wa kijiji cha Ibole kata ya Igurubi wilayani hapa.

Tukio hilo lilitokea Desemba 25 majira ya saa 7:30 jioni katika kijiji cha Ibole kata ya Igurubi wilayani hapa ambapo watuhumiwa hao ambao ni wajukuu walimpiga babu yao Makelemo Jagadi (55) na kusababisha kifo chache.

Inadaiwa kuwa marehemu alikuwa amelewa pombe na alipofika nyumbani alianza kutukana hali ambayo ilipelekea kuanza kupigana na mke wake Milembe Mpela(50) na ndipo wajukuu zake walipoingilia ugomvi huo.

Aidha wakiwa katika ugomvi huo watuhumiwa hao walimpiga Babu yao Makeremo kwa kitu kizito kichwani kwenye paji la uso pamoja na kumvunja mkono wa kushoto na kusababisha kifo hicho.

Diwani wa kata ya Igurubi Bw.Edson Sadani alisema kuwa kufuatia ugomvi huo pia mke wa marehemu huyo aliumia na kusema kuwa amelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Igunga kwa matibabu.

Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora kamishna msaidizi Peter Ouma alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa watuhumiwa hao bado wanashikiliwa na polisi na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma zinazowakabili.

This entry was posted in

Leave a Reply