Google PlusRSS FeedEmail

BAADA YA KUZINDULIWA KADI ZA B-PESA SASA KAMPUNI YAJA NA 'MSHAHARA CARD'

DAR ES SALAAM, Tanzania
MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni  ya Smart Banking Solutions (SBS) Gustav Vermaas, amesema baada ya kampuni hiyo kuingiza sokoni hivi karibuni kadi yake ya B-PESA sasa ina mpango wa kuzindua kadi itakayoitwa ‘mshahara card’ ili kurahisisha maisha ya wafanyakazi  nchini.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Veremaas alisema lengo la kadi hiyo ni kumwezesha mfanyakazi kutopata usumbufu wa kwenda kupanga foleni kuchukua mshahara wake benki.

 Vermaas alisema kadi ya mshahara itamwezesha mfanyakazi kupata msahahara wake moja kwa moja pindi unapoingizwa benki na taarifa atazipata kupitia simu yake ya mkononi.

“Lakini pia, tuna mkakati wa kuhakikisha kuwa kila sehemu yenye wafanyakazi wengi, mwajiri akikubali mpango huu tunaweka mashine za kutolea huduma ya B-PESA,”alisema.

Alisema kwa kufanya hivyo, mfanyakazi atakuwa na uhakika wa kupata fedha zake karibu na hatapoteza muda, badala yake atakijikita katika kutekeleza majukumu yake kama kawaida.

Alisema kadi ya B-PESA inaruhusu kuwa na matumizi mengi ikiwemo uhamisho wa fedha kwenye kadi, kutolea fedha, kuingiza fedha, na kulipia bili,kununua bidhaa na kulipa huduma mbalimbali.

Vermaas alisema kuwa kadi hiyo ni salama na ina hadhi ya kibenki.”Fedha kwenye kadi ya B-PESA zinakuwa salama kwa sababu kadi hiyo hutumia teknolojia ya kisasa na bora yenye kudhibiti na kulinda namba ya siri,”alieleza.

This entry was posted in

Leave a Reply