Google PlusRSS FeedEmail

JAJI WARIOBA KUKABIDHI RASIMU KWA RAIS KIKWETE, DK. SHEIN JUMATATU HII

JAJI WARIOBA
DAR ES SALAAM, Tanzania
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Tume ya Mabadiliuko ya Katiba, Assaa Rashid, imesema, Jumatatu ijayo ya Desemba 30, 2013, Tume hiyo itakabidhi rasimu hiyo kwa Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.

"Tume inapenda kuwafahamisha wananchi na wadau wengine kuwa hafla ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi itafanyika siku ya Jumatatu, Desemba 30, 2013 saa 6:00 mchana katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam", taarifa hiyo imesema.
Taarifa imesema, hafla hiyo pia inatarajiwa kuhudhuriwa na Viongozi wa Serikali, Vyama vya Siasa, Taasisi za kidini, Asasi za kiraia na wananchi wa kawaida.
Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba anatarajia kuwakabidhi Waheshimiwa Marais, ripoti ya mchakato wa Katiba na rasimu ya Katiba.
Rasimu hiyo ya Katiba imetokana na maoni ya wananchi, viongozi na makundi mbalimbali waliyowasilisha kwa Tume kupitia njia mbalimbali zikiwemo mikutano, barua pepe, anuani za posta, Tovuti ya Tume na ukurasa wa facebook wa Tume (Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania).

This entry was posted in

Leave a Reply