Google PlusRSS FeedEmail

RAIS KIKWETE AMTEUA ERNEST MANGU KUWA MKUU MPYA WA JESHI LA POLISI (IGP), ABDULRAHMAN KANIKI NAIBU IGP

NA BASHIR NKOROMO, DSM
Amirijeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Tanzania, Rais Jakaya Kikwete Jumatatu, Desemba 30, 2013, amemteua Kamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, imemkariri Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, akisema kuwa Kamishna Mangu (pichani) anachukua nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini anayestaafu, Saidi Mwema.

"Kabla ya uteuzi wake unaoanza keshokutwa, Januari Mosi, 2014, Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai (Director of Criminal Intelligence) katika Jeshi hilo la Polisi", tarifa hiyo imesema.

Taarifa hiyo imesema kuwa pia Rais Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.

Kabla ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner for Forensic Investigations).

Taarifa hiyo imesema, Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya ataapishwa Jumanne,  Desemba 31, 2013 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.

This entry was posted in

Leave a Reply