Google PlusRSS FeedEmail

CCM MOROGORO WAFAGILIA ZIARA ZA KINANA MIKOANI, NI KATIKA SEMINA YA VIONGOZI WA JUMUIA YA WAZAZI KINONDONI

 
 Mgeni rasmi, Dorothy Mwamsiku akiingia ukumbini huku akisindikizwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge na Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi ya CCM Kinondoni, Charles Mgonja.
 Mgeni rasmi akiwa na viongozi wa Jumuia ya Wazazi na CCM, baada ya kuingia ukumbini
 Madenge akizungumza kabla ya semina kufunguliwa
 Dorothy akifungua semina hiyo
 Baadhi ya wajumbe wakiwa ukumbini kwenye semina hiyo
 Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mada kwenye semina hiyo
 Mmoja wa wajumbe akiwahamasisha wenzake baada ya semina kufunguliwa
Madenge akiagana na Dorothy baada ya semina kufunguliwa.

HABARI KAMILI

CCM MORO WAPONGEZA ZIARA ZA KINANA MIKOANI
*Mwenezi asema zianaimarisha, kujenga heshima ya chama
*Ataka Wana-CCM kuunga mkono ziara hizo 

BASHIR NKOROMO NA LATIFA GANZEL, MOROGORO
CHAMA cha Mapinduzi CCM mkoa wa Morogoro kimepongeza ziara za katibu mkuu wa CCM Abduraharam  Kinana kwamba ziara hizo zimezidi kukiimarisha chama na kukiongezea heshima.

Katibu wa Itikadi na uenezi wa mkoa wa Morogoro Dorothy Mwamsiku alisema hayo wakati akifungu semina ya viongozi wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM,  wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, leo, katika ukumbi wa Road View Motel iliopo Nane nane manispaa ya Morogoro.

Aliwataka wanachama wa CCM nchi nzima kumuunga mkono Kinana na Sektetarieti yake kwa kusimamia na kutekeleza maagiizo aliyotoa katika ziara hizo ikiwemo kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM na kisikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kusitatua.

Katibu huyo alisema kuwa kuna kila sababu ya viongozi wa CCM kutokubali kuwafumbia macho watendaji wanaoshindwa kutekeleza ilani ya CCM kwa makusudi kwa lengo la kukikwamisha chama hiki.

Alisema   kuwa wapo watendaji ambao hawakitendei haki chama cha  Mapinduzi kwa, kufuja  fedha za miradi kwa makusudi .

'' Unakuta baadhi ya watendaji hawatekelezi ilani ya CCM ipasavyo na hivyo kusababisha CCM kusemwa vibaya, tusikubali, sisi tuwe wakwanza kuwashughulikia kabla ya sisi kunyoshewa vidole'' Alisema.

Hata hivyo alisema kuwa kuna kila sababu kwa viongozi wa CCM na wanachama kwa ujumla wanatambua miradi yote ya maendeleo iliopo ktika maeneo yao inavyoanza kutekelezwa ili ikitokea mtendaji anafanya ubadhilifu iwe rahisi kuwashughulikia.

Aidha alisema kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali za baadhi ya watendaji wanaokwamisha utekelezaji huo wa ilani lakini  hadi sasa ilani hiyo imetekelezwa kwa kiasi kikubwa.
"Pamoja na utekelezaji huo bado wapo watu wanaosema CCM haijafanya kitu, kazi ya wapinzani kukosoa  na CCM kazi yatu kutenda, tusikate tamaa tusonge mbele.

Aliwataka jumuiya ya wazazi kuwa mstari wa mbele katika malezi ya watoto kwa kuwa hiyo ndio moja ya malengo ya kuanzishwa kwa jumuiya hiyo badala ya kuwaachia vijana wakiharibika na kutumbukia katika vitendo viovu vinavyopelekea kupata maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi.

Kwa upende wake Mwenyekiti wa CCM wilaya Kinondoni, Salumu Madenge ambaye ndiye Mwenyekiti wa semina hiyo, alisema,  lengo la semina hiyo ni kuwaweka viongozi hao katika mazingira ya ulelewa wa kutosha wa namna mbalimbali ya kutekeleza majukumu yao na wajibu wa kwa chama cha Mapinduzi.

Awali mwenyekiti wa wazazi wilaya ya Kinondoni Charlse Mgonja alisema  katika semina hiyo mada mbalimbali zitatolewa ikiwemo umuhimu wa mchango wa jumuiya hiyo katika kuimarisha chama cha Mapinduzi, na historia na kusimamia maadili ya wanachama na viongozi ili kuimarisha umoja na mshikamano ndani ya CCM na jumuiya zake.

This entry was posted in

Leave a Reply