KATIBU MKUU WA CCM KINANA |
CHAMA Cha Mapinduzi CCM, Mkoa wa Dar e s salaam, leo jumapili kimeandaa mapokezi makubwaya Katibu Mkuu wao, Abralrahaman Kinana , kufuatia kumaliza ziara katika Mikoa mitatu ya Ruvuma, Mbeya na Njombe kwa mafanikio makubwa.
Kinana na ujumbe wake akiwemo Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Katibuwa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha Migiro watapokelewa katika Stesheni ya Tazara jioni .
Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Dar e s salaam, Juma Simba amewambia waandishi wa habari kuwa katika mapokezi hayo kutakuwa na Burudani kutoka kwa Wasanii mbalimbali wa muziki wa Kizazi Kipya.
Kutokana na mapokezi hayo, CCM imetoa wito kwa Wananchi pamoja na wana-CCM kujitokeza kwa
wingi katika mapokezi hayo.
Katika Mikoa ambayo Katibu Mkuu wa CCM, ameweza kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili
wananchi na kuzitolea ufafanuzi ikiwa ni pamoja na kuwaelekeza mawaziri husika kutokaa ofisini na
badala yake weende vijijini kuwasikiliza wananchi. : IMETAYARISHWA NA UHURU FM-DSM