Google PlusRSS FeedEmail

MWALIKO KWA MAKUNDI MBALIMBALI KUPENDEKEZA MAJINA YA WATAKAOTEULIWA KUWA WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
TANZANIA INFORMATION SERVICES
 PRESS RELEASE
               P.O. Box 9142, Dar es Salaam, Tel:  2110585, 2122771/3, Fax: 2113814, e-mail:

Date:  20/12/2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MWALIKO KWA MAKUNDI MBALIMBALI KUPENDEKEZA MAJINA YA WATAKAOTEULIWA KUWA WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  anapenda kutoa mwaliko kwa makundi mbalimbali kwa ajili ya kuwasilisha orodha ya watu wasiopungua wanne na waziozidi tisa kwa ajili ya kuteuliwa kuwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (2A) cha kifungu cha 22 cha sheria ya Mabadiliko ya Katiba, sura ya 83 kinachomtaka Rais kuwaalika kila kundi lililoainishwa chini ya kifungu kidogo cha (1) (c) kutoka pande zote za Muungano kuwasilisha kwake orodha ya majina yasiyopungua 4 na yasiozidi 9 kwa ajili ya kuzingatiwa katika uteuzi.

Makundi hayo ni kama ifuatavyo:

Taasisi zisizokuwa za Kiserikali
Taasisi za kidini
Vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu
Taasisi  za elimu ya juu
Makundi yenye ulemavu
Vyama vya wafanyakazi
Vyama vinavyowakilisha wafugaji
Vyama vya wakulima
Vyama vinavyowakilisha wavuvi
Makundi mengine yenye malengo yanayofanana

Katika kuwasilisha majina hayo, makundi yaliyoalikwa yatalazimika kuonesha umri, jinsia, uzoefu, sifa na sehemu ya makazi ya mtu aliyependekezwa ikiwa ni pamoja na kuzingatia usawa wa kijinsia.

Mheshimiwa Rais ameelekeza kuwa orodha ya majina yanayopendekezwa yawasilishwe kwa maandishi ama kwa kupeleka kwa mkono au kutumia huduma ya posta kwa anuani zifuatazo:

Katibu Mkuu Kiongozi,
Ofisi ya Rais, Ikulu,
S.L.P. 9120,
DAR ES SALAAM

Katibu Mkuu Kiongozi,
Ofisi ya Rais,
S.L.P. 4224,
ZANZIBAR

Mwisho wa kupokea orodha ya majina hayo nitarehe 02 Januari, 2014.

This entry was posted in

Leave a Reply