Google PlusRSS FeedEmail
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba za Walimu wa Shule ya Sekondari ya Mwakaleli.
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akikata ubao akiwa pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakikata mbao kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya maabara na madarasa ya shule ya Sekondari ya Mwakaleli.
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiongea na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mwakaleli na kuwataka wanafunzi waongeze bidii kwenye masomo kwani elimu haina mwisho.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimu wanafunzi wa  shule ya sekondari ya Mwakaleli baada ya kumaliza kushiriki shughuli za kimaendeleo ya ujenzi wa madarasa ,maabara na nyumbza za walimu.
 Mbunge wa Jimbo la Rungwe Magharibi Profesa David Mwakyusa akiwasalimu wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwakaleli na kuwataka wajitahidikusona na kuepukana na vitendo vitakavyo waharibia maisha yao.
 Wanafunzi wa Kidato cha Sita wa shule ya Sekondari ya Mwakaleli wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Mahusiano ya Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro na Mbunge wa Viti maalum wanawake mkoa wa Mbeya Dk.Mary Mwanjelwa.
 Mzee Issa Simion akitoa salaam kwa niaba ya wazee wa Kijiji cha Katende na pia kushukuru kwa Serikali na Chama Cha mapinduzi na pia kuelezea kero zinazohusu wakazi wa kata ya Katende.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Katende ambapo alihimiza sana kuwa makini na vyama vinavyojita vya siasa  kwani sasa vimeanza kupoteza muelekeo.
Mbunge wa Wanawake Mkoa wa Mbeya  Dk.Mary Mwanjelwa akiwasalimia wakazi Katende
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na wazee wa kijiji ambao leo walimpa heshima ya kuwa Mzee wa Katende na kumvisha mgolole kama heshima ya mtu mzima.
 Katibu wa NEC Siasa na Mahusiano ya Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwa ameketi kwenye mkeka unaojulikana kama Kalili aliopewa zawadi na wakina mama wa Katende.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Katende na kuwaahidi CCM inatekeleza ilani yake ya uchaguzi na kusema ahadi zilizoahidiwa zitatimizwa.
Katibu Mkuu wa CCM aliwaambia wananchi hao kuwa lazima tuhoji serikali  pesa za maendeleo kwa nini haziji kwa wakati.

WATENDAJI WATAKIWA KUTUMIKIA WANANCHI

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba za Walimu wa Shule ya Sekondari ya Mwakaleli.   Katibu wa NEC Siasa... [Read More]

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika kata ya Ipinda, wilayani Kyela mkoani Mbeya, Nov 24, 2013, alipowasili katika kata hiyo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kushirikiana nao njia ya kuzitatua.
 Maelfu wa wananchi wakimsikiliza Katibu wa NEC, Itikadi na Unezi Nape Nnauye kwenye mkutano wa CCM uliofanyika Kata ya Ipinda, wilayani Kyela mkoani Mbeya, Nov 24, 2013.
 Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe akihutubia maelfu ya wananchi katika kata ya Ipinda, wilayani Kyela mkoani Mbeya, Nov 24, 2013, Wakati Katubu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipowasili katika kata hiyo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kushirikiana nao njia ya kuzitatua.
 Katibu Mkuu wa CCM, akikagua mradi wa maendeleo ya Ujenzi wa jengo la huduma za wenye virusi vya Ukimwi,katika Hospitali ya wilaya ya Kyela mkoani Mbeya, Nov 24, 2013, alipowasili katika wilaya hiyo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kushirikiana nao njia ya kuzitatua. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya, Maganga Sengerema na Katibu wa NEC, Itikati na Uenezi Nape Nnauye.
 Baba, Raphael Simon (kulia) na mtoto wake, Simon Raphael waliokuwa wanachama wa Chadema, wakiwa na kadi za Chama hicho kabla ya kumkabidhi Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati), katika mkutano  wa shina, uliofanyika nyumbani kwa  Mjumbe wa shina la Menasi Ndoma, Kata ya Matema, Kyela mkoani Mbeya, Nov 24, 2013.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akiwa na Mjumbe wa Shina, Menas Ndomba, baada ya kuwasili nyumbani kwa mjumbe wa shina hilo, katika kata ya Matema, wilayani Kyela mkoani Mbeya, Nov 24, 2013. alipowasili katika kata hiyo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kushirikiana nao njia ya kuzitatua.
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa KImataifa, Dk. Asha-Rose (watatu kushoto waliokaa), na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (katikati) wakiwa na wananchi, nyumbani kwa mjumbe wa shina,  Nemas Ndoma, Kata ya Matema, wilayani Kyela mkoani Mbeya, Nov 24, 2013, wakati Katibu Mkuu wa CCM alipowasili nyumbani kwa mjumbe huyo wa shina, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kushirikiana nao njia ya kuzitatua.
 Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mbeya Dk. Mary Mwanjelwa, akilala chini mbele ya wananchi nyumbani kwa mjumbe wa shina, Menasi Ndoma, kuwashukuru kwa mapokezi mazuri ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia), alipowasili katika shina hilo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kushirikiana nao njia ya kuzitatua.
Kupenda watoto: Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akichezea 'kigari' cha watoto Asifiwe Mwambene na John Asimwisye, alipokutana nao njiani akiwa katika ziara, ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kushirikiana nao njia ya kuzitatua, katika Kata ya Matema, wilayani Kyela mkoani Mbeya, Nov 24, 2013.

ZIARA YA KINANA YATIKISA KYELA, MAELFU WAFURIKA MIKUTANO YAKE, AKATA VICHOCHORO HADI KWA WAJUMBE WA MASHINA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika kata ya Ipinda, wilayani Kyela mkoani Mbeya, Nov 24, 2013, alip... [Read More]

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi, baada ya kuwasili katika bandari ndogo ya Kiwira, wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov 24,2013.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana 'akiwasaluti' Wananchi baada ya kuwasili katika bandari ya Kiwira, wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov 24, 2013. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Maganga Sengerema na kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiri (kulia), wakishuka kutoka katika mv Songea, baada ya msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kuwasili katika bandari ndogo ya Kiwira, wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov 24, 2013.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Godfrey Zambi, baada ya kushuka katika Mv Songea, baada ya kuwasili katika bandari ndogo ya Kiwira, wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov 24, 2013.
 Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe akimlaki wa furaha, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipompokea katibu mkuu huyo, baada ya kuwasili katika bandari ndogo ya Kiwira, wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov 24, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwapungia mkono wananchi, baada ya kuwasili katika bandari ndogo ya Kiwira, wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov 24,2013.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (Kushoto, aliyenyoosha mkono) akikagua kivuko katika bandari ya zamani ya Itunge, baada ya kuwasili  wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov 24, 2013. Bandari hiyo ambayo imekufa kwa miaka mingi sasa, ipo katika mpango wa kufufuliwa na serikali.
 Nahodha wa mv Songea Tom Faya akimpatia maelekezo ya namna meli hiyo inavyofanya kazi, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake, wakati katibu mkuu huyo alipokuwa  akisafiri na meli hiyo kutoka Mbamba Bay mkoani Ruvuma kwenda Kyela mkoani Mbeya, leo Nov 24,2013. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Siasa na Uhisiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro. Kwenye usukukani ni Nahodha Msaidizi, Conrad Shauritanga.
Baadhi ya abiria waliosafiri na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana katika mv Songea, alipokuwa alitokea Mbamba Bay mkoani Ruvuma kwenda Kyela mkoani Mbeya. Meli hiyo iliyoanza kazi katika Ziwa Nyasa, mwaka 1974, ina uwezo wa kubeba abiria 213 wakiwemo wafanyakazi 13 wa meli hiyo.

KINANA AWASILI KYELA BAADA YA SAFARI YA ZAIDI YA SAA 24 KWA MELI KUTOKA MBAMBA BAY MKOANI RUVUMA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi, baada ya kuwasili katika  bandari ndogo ya Kiwira, wilayani Kyela mkoani Mb... [Read More]

 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, asubuhi hii amemaliza ziara yake katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma na kuanza safari ya kwenda Kyela ambako ataanza ziara katika mkoa wa Mbeya. Pichani, Kinana na wajumbe wa sekretarieri ya CCM, Nape Nnauye (Itikadi na Uenezi) na Dk. Asha-Rose Migiro (Siasa na Uhusiano wa KIImataifa), wakiwapungia mikono wananchi wa Nyasa, baada ya kupanda Mv Songea katika bandari ndogo ya Mbamba Bay, kuanza safari ya kwenda Kyenla. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Nyasa, Ernest Kahindi 
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na wananchi wa Mbamba Bay, Nyasa, kabla ya kupanda meli kwenda Kyela
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migirob akisalimiana na Nahodha wa Mv Songea Tom Faya, katika bandari ndogo ya Mbamba Bay, wilayani Nyasa mkoani Ruvuma kabla ya safari ya kwenada Kyela
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Nahodha wa mv Songea, kabla ya safari ya kwenda Kyela kutoka bandari ndogo ya Mbamba Bay, Nyasa. Wapili kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa Oddo Mwisho
 Mkurugenzi na Mtayarishaji Mkuu wa theNkoromo Blog, Bashir Nkoromo, ambaye ni baadhi ya abiria walioko katika msafara wa Kinana,akipanda mv Songea.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akipanda mv Songea. Wanaomfuata na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho na katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
 Wananchi na wanachama wa CCM wa Mbamba Bay, wilayani Nyasa mkoani Ruvuma, wakisindikiza kwa boti mv Songea wakati ikiondoka bandarini
Nahodha wa ,mv Songea na Kinana wakizungumza na waandishi wa habari. Imetayarishwa na theNkoromo Blog

KINANA AMALIZA ZIARA WILAYANI NYASA, AKWEA MELI KWENDA KYELA KUENDELEA NA ZIARA MKOANI MBEYA

  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, asubuhi hii amemaliza ziara yake katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma na kuanza safari ya kwenda Ky... [Read More]

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya jinsi ya kutumia vifaa vya maabara katika kufanikisha kutambua kemikali kutoka kwa wanafunzi wa kidato cha nne Erasto Ndumba na Stella Hyera wa shule ya sekondari ya Kata ya Mtakatifu Paul kata ya Liuli wilaya ya Nyasa
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi nyumba za madaktari zilizochini ya mradi wa Taasisi Benjamini Mkapa katika kituo cha afya  Mkili kata Liundi wilayani Nyasa.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishauri jambo kabla ya kuvuka mtu Ruhuhu kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Mwenyekiti wa CCM Ndugu Oddo Mwisho.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Ndugu Ernest Kahindi wakivuka kwa mtumbwi kuelekea kijiji cha Kipingu wilaya ya Ludewa.
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimu wakazi wa kijiji cha Kipingu wilayani Ludewa, Kijiji hicho kipo mpakani wa mkoa wa Ruvuma na Njombe.

Katibu Mkuu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa kata Kipingu kijiji cha  Kipingu wilaya ya Ludewa ambapo aliwaambia ahadi ya kujengwa kwa daraja la mto Ruhuhu, uzalishaji wa umeme utakotosheleza mahitaji ya  wilaya ya Nyasa na Ludewa pamoja na mradi wa umwagiliaji.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipungia wananchi wakati akirejea kijiji cha Lituhi kwa Mtumbwi  baada ya kutoka kuwasalimu wakazi wa kijiji cha Kipingu wilayani Ludewa,wengine pichani ni Dk.Asha-Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na kikundi cha akina mama wakulima wa mpunga na mboga mboga wa kijiji cha Lituhi katika viwanja vya Lituhi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma Verena Shumbusho wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa  Mbinga Magharibi Kapteni John Komba wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya mikutano Lituhi ambapo vijana 12 kutoka vijiji mbali mbali walipewa mabati kwa ajili ya kuezeka nyumba zao.
 Mbunge wa Mbinga Magharibi Kapteni John Komba akimtambulisha Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kama Ndugu yake wa karibu kwani mafanikio yake yametokana na mchango mkubwa wa Marehemu Mzee Nnauye ,Pia Komba alimuelezea Kinana kama mmoja wa walimu wake wazuri wa masomo ya kijeshi pamoja na siasa.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akionyesha kadi za wanachama  wa Chadema waliorudi CCM baada ya chama chao kuanza kuparanganyika,mkutano huo uliofanyika kwenye viwanja vya Lituhi ambapo wanachama zaidi ya 400 wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanachama waliojiunga na CCM kutoka vyama vya upinzani.

KINANA AVUNA WANACHAMA KIBAO KUTOKA UPINZANI

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya jinsi ya kutumia vifaa vya maabara katika kufanikisha kutambua kemikali kuto... [Read More]