Google PlusRSS FeedEmail

SAKATA LA RUZUKU: NAPE ASEMA CCM IMEKAGULIWA NA HAINA HAJA YA KULUMBANA

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Nape Nnauye.



Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Nape Nnauye ameeleza

kuwa Chama Cha Mapinduzi kimekaguliwa na ushahidi wa ukaguzi huo upo. Na akabainisha kuwa amesikitishwa na kauli za Naibu Katibu Mkuu Chadema na Mwenyekiti wa PAC Mheshimiwa Zitto Kabwe juu ya shutuma zake na muendelezo wa kauli zake juu ya Chama hiko.



Nukuu ya Nape ni hii;


   "..Nimesikitishwa na vitisho vya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya PAC kuwa eti hatustahili kujibu tunapotuhumiwa.!! Si demokrasia wala si sheria kutuhumu halafu unaowatuhumu wasiwe na haki ya kujieleza. Kama Sheria hiyo ipo nitaishangaa sana! Na sina muda wala sababu ya kulumbana lakini ninaamini tuna haki ya kueleza ukweli wa hali halisi

hakuna sababu ya kuvutana katika hili, sie tunao ushahidi wa kukaguliwa na Kampuni iliyoteuliwa na CAG na hatujaanza jana kukaguliwa toka mwaka 1977/78 tunakaguliwa. Kukaguliwa kwetu ni sehemu ya maisha yetu kwa sasa, tuko tayari kukutana na kamati ya bunge kwani hesabu zetu ni safi! Ni vyema Zitto akatimiza wajibu wake na kusimamia sheria bila vitisho.

Niko tayari kufungwa kwa kusimamia utawala wa sheria na kuhakikisha haki hata kama ni ya mtuhumiwa inazingatiwa. Kama yeye alivyotayari kunyongwa kwa kusimamia sheria. Sipingani naye kwenye kusimamia Sheria, lakini naamini kama taasisi tuna haki ya kujitetea tunapotuhumiwa na kujitetea sio kulumbana.."






This entry was posted in

Leave a Reply