Google PlusRSS FeedEmail
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye akiangalia matunda ya Mchikichi ambayo yanachemshwa katika mapipa kwaajili ya kukamua mafuta ya mawese katika Kijiji cha Ilagala, Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.
 Wana CCM wa Igalula wakiwa katika kikao cha ndani na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye akikagua maendeleo ya ujenzi katika Kituo cha afya Ilagala.
 Nyumba ya Daktari wa Ilagala
 
Wakazi wa Ilagala wakimsikilaza Nape Nnauye
 Nape akihutubia wakazi wa Ilagala ambao walitoa kilio chao kuwa ni mgogoro wa ardhi baina ya Kijiji na Magereza .

NAPE AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO ILAGALA KIGOMA

  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye akiangalia matunda ya Mchikichi ambayo yanachemshwa katika mapipa kwa... [Read More]

* Wanaosema inawezekana wanawadangaya wananchi
* Asema yenyewe inafungua funsa tu
* Wanaokwanza Kilimo Kwanza ni wezi, waadhibiwe
NA BASHIR NKOROMO, KIGOMA
KATIBU Mkuu wa CCM, amewataka Watanzania kuacha kujidanganya au kudanganywa na mwanasiasa yeyote kwamba kuna serikali itakayoweza kutoa ajira kwa kila mtu na kwamba kuamini hivyo ni kupumbazwa kifikra..

Alisema, badala yake serikali zote ikiwemo ya Tanzania inayosimamiwa na CCM, kazi yake ni kuandaa na kuweka mazingira na fursa bora zinazowezesha wananchi kufanya kazi mbalimbali za kuweza kuinia uchumi wao na wa taifa kwa jumla.

Kinana alisema hayo kwa nyakati tofauti, akizungumza kwenye mkikuatano ya hadhara, katika wilaya mpya ya Kakonko, akiwa katika ziara mkoani Kigoma, ambayo ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM zinazofikia kilele chake, Februari 3, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.

Alisema, kutokana na kutambua hilo, serikali ya Chama Cha Mapinduzi, imekuwa ikifanya jitihada za kuweka mazingira bora ya amani na utulivu hapa nchini ili kila mtu aweze kufanya shughuli zake bila bughudha wala kulazimika kukimbia eneo lake kwenda lingine kwa hofu ya kupoteza maisha.

Kinana alisema, pamoja na kuimarisha amani, Serikali imekuwa ikibuni fursa mbalimbali kuwezesha wananchi kujiajiri hasa katika sekta binafsi, ikiwemo katika  viwanda na kilimo huku akisisitiza kwamba kwa kutambua kwamba kilimo ndicho kinachotoa ajira kwa watu wengi kwa zaidi ya asilimia 75, nguvu kubwa ya serikali imeelekezwa kwenye sekta hiyo.

"Tunatambua na kuamini kwamba asilimia kubwa ya waliojiajiri wapo kwenye sekta ya kilimo, ndiyo sababu serikali yenu ya CCM, imeupa umuhimu mkubwa mpango wa Kilimo kwanza ili sekta hii iweze kuwa ya mafanikio makubwa na hivyo kuweza kuinua maisha ya watu na taifa kwa jumla", alisema Kinana.

Kinana ambaye wilayani Kakonko alihutubia mikutano mbalimbali ya ndani na ya hadhara, alisema, serikali imekuwa ikiimarisha mpango wa Kilimokwanza kwa kuhakikisha wakulima wanalima kilimo cha kisasa na chenye tija, kwa kuwapatia maarifa, zana na pembejeo.

Hata hivyo Kinana alisema, wakati serikali imo katika jitihada hizo, wapo baadhi ya watu walipoewa jukumu la kusimamia usambazaji wa pembejeo wamekuwa kikwazo kikubwa kwa kwenda kinyume na inavyotakiwa na hivyo kufifisha matarajio.

"Inashangaza kwamba kuna baadhi ya wafanyabiashara ambao kampuni zao zimepewa jukumu la kusambaza pembejeo kama mbolea kwa wakulima hapa Kakonko, lakini wanafanya hujuma kwa kuchelewesha mbolea na wanapoifikisha inakuwa si kwa kiwango kinachotakiwa", alisema Kinana.

"Kwa kweli hawa wanapswa kuitwa wezi, kwa sababu hawakiuki kwa makosa bali kwa makusudi kwa ajili ya ubinafsi wa kutaka kujinufaisha wao jambo ambalo lazima serikali ya CCM ichukue hatua za haraka kuwadhibiti ikiwemo kuwachukulia hatua za uhakika za kisheria wahusika", alisema.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Kasanda wilayani Kakonko,
Diwani wa Kata hiyo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibondo ambayo ndiyo kwa sasa inasimamia shughuli za wilaya hiyo mpya ya Kakonko, Juma Maganga alimwambia Kinana kwamba, baadhi ya wafanyabiashara waliopewa jukumu la kusambaza pembejeo za kilimo hawatimizi wajibu wao kwa wakulima.

Alisema, baadhi wamekuwa wakipeleka kwa wakulima mbolea ya kukuzia kabla ya ile ya kupandia ambayo ndiyo inatakiwa kutangulia kwanza, na mmoja wa wafanyabiashara hao alipeka kwa wakulima magunia 20 tu ya mbolea badala ya 180 yaliyokuwa yanahitajika.

Pamoja na mikutano ya hadhara, Kinana amekagua shughuli za maendeleo, ikiwemo uenzi wa nyumba za zahanati katika kata ya Kasanda, ujenbzi wa daraja la Umoja katika mpaka wa Tanzania na Burundi kwenye kijiji cha Nyabibuye, Kakonko ambacho kinapakana na mkoa wa Changuzo ulioko Burundi.

Daraja hilo linalotarajiwa kukamilika Machi mwaka huu, linalengwa kuchangamsha biashara zitakazofanywa baina ya warundi na Watanzania kwenye soko jipya na la kisasa linalojengwa na wizara ya Kilimo na chakula katika kijiji cha Nyabibuye.

Kinana pia ameshiriki ujenzi wa nyumba mbili za walimu unaoendelea katika shule ya sekondari ya Nyamtukuza iliyopo kata hiyo, ambapo alishirikina na wananchi, walimu na wanafunzi kusomba mawe kwa ajili ya ujenzi huo

Wakati Kinana anafanya ziara katika wilaya za Kakonko na Kibondo, wajumbe wengine wa sekretarieti aliowasili nao mkuani Kigoma kwa ajili ya sherehe hizo za miaka 36 ya CCM wapo katika wilaya za Kasulu na Kigoma vijijini kuhamasisha maendeleo na kugagua utekelezaji wa ilani ya CCM.

KINANA: SERIKALI HAIWEZI KUAJIRI KILA MTU

* Wanaosema inawezekana wanawadangaya wananchi * Asema yenyewe inafungua funsa tu * Wanaokwanza Kilimo Kwanza ni wezi, waadhibiwe NA BASHIR... [Read More]

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana leo amedhihirisha kuwa ni mtu wa vitendo zadi kuliko maneno, baada ya kuonyesha uwezo wake wa kufanya kazi za kijamii kwa umahiri mkubwa, kwa kushiriki katika ujenzi wa chumba cha darasa katika shule ya Sekondari Kumwambo   na ujenzi wa Ofisi ya CCM tawi la Bunyambo, akiwa katika ziara kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama, ambayo ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM, ambayo kilele chake ni Februari 3, mwaka huu mjini Kigoma. Pichani Kinana akishiriki ujenzi wa darasa katika shule ya sekondari Kumwambo, Kibondo
 Kinana akiongoza ujenzi wa chumba cha darasa kwenye shule ya sekondari Kumwambo. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Abdallah Bulembo na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dk. Amani Walid Kaborou
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananfunzi wa shule hiyo baada ya kushiriki ujenzi huo. Baadaye Kinana alienda na msafara wake Kijiji cha Bunyambo ambako pia alishiriki ujenzi wa Ofisi ya tawi la CCM na kuahidi kuwapa sh. milioni 2 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi.
 Kinana akiongoza ujenzi wa Ofisi ya CCM tawi la Bunyambo, wilayani Kibondo mkoani Kigoma
 Kinana akihakiki kwa kipimo wakati akiendelea na ujenzi kwenye ofisi hiyo ya CCM. Kulia ni Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Kigoma, Stanley Mkandawile
 Kinana akiendelea na ujenzi kwenye Ofisi hiyo ya CCM
 Kinana akitazama kama tofali limekaa sawa, wakati akishiriki kujenga Ofisi hiyo ya CCM

 LETE TOFALI: Anasema Kinana kumwabia Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dk. Kaborou wakati akiendelea kushiriki ujenzi wa Ofisi hiyo ya CCM
Kisha Kinana akawaaga wananchi waliohudhuria kwenye Ujenzi wa Ofisi hiyo
Katibu Mkuu wa CCM (kushoto) na ujumbe wake wakichagua miwa kwa muuzaji waliyemkuta njiani wakati wakitemebea kwa mguu kiasi cha kilometa moja na nusu kwenda kwenye mkutano wa hadhara baada ya ujenzi huo. (PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO)

KINANA WEE ACHA TU, ASHIRIKI KIKWELI UJENZI WA MIRADIDUNDO UJENZI WA MIRADI KIBONDO

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana leo amedhihirisha kuwa ni mtu wa vitendo zadi kuliko maneno, baada ya kuonyesha uwezo wake wa kufan... [Read More]

 Wananchi wa Kijiji cha Kilemba wilayani Kibondo mkoani Kigoma, wakiserebuka kwa ngoma mbele ya Katibu Mkuu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kushoto) na ujumbe wake, alipoowasili kwenye kijiji hicho nje kidogo ya mji mdogo wa Kibondo leo asubuhi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Bulembo na watatu ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Amani Kaborou.
 Msafara wa Kinana ukiingia mjini Kibondo kwa shamrashamra za aina yake. (PICHA NA BASHIR NKOROMO)

KINANA AINGIA KWA KISHINDO KIBONDO LEO

 Wananchi wa Kijiji cha Kilemba wilayani Kibondo mkoani Kigoma, wakiserebuka kwa ngoma mbele ya Katibu Mkuu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ... [Read More]

 Mtoto akitafuta wateja wa miwa kwenye stesheni ya Kazutramimba mkoani Kigoma, hivi karibuni
 Ally Bikulako mkazi wa Nguruka wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, akiwa katika kazi ya ufundi wa kuchora bango la shule ya sekondari ya Nguruka, hivi karibuni.
 Mamalishe wakiwa kazini katika kijiji cha Nguruka, wilayani Uvinza mkoani Kigoma hivi karibuni.
 Mafundi wakiwa katika ujenzi wa nyumba ya kisasa katika Kijiji cha Kasanda, wilayani Kakonko mkoani Kigoma juzi.
 Watoto wakichota maji safi ya bomba kwenye kijiji cha Nyabibuye, Kakonko mkoani Kigoma jana.
 Belitha Anthoy wa Kijiji cha Lumashi, Kata ya Nyabibuye, Kakonko mkoani Kigoma akichoma mahindi, nyumbani kwao, jana. Huu ni msimu wa mahindi mabichi Kigoma
 MTOTO akiswaga mbuzi aliokuwa anachunga katika kijiji cha Malagarasi, wilayani Uvinza mkoani Kigoma, juzi.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

WATU NA MATUKIO KIGOMA

 Mtoto akitafuta wateja wa miwa kwenye stesheni ya Kazutramimba mkoani Kigoma, hivi karibuni  Ally Bikulako mkazi wa Nguruka wilaya ya Uvinz... [Read More]

RAIS KIKWETE AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS KABILA IKULU

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kabla ya kufanya naye mazungumz... [Read More]

 Wananchi wa rika zote wa Kijiji cha Rumashi, Kata ya Nyabibuye, wilayani Kakonko, Kigoma wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahma Kinana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo, Januari 30, 2013,katika  kijiji hicho, ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu inayoambana na maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake ni Februari 3, mwaka huu mjini Kigoma.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Rumashi, Kata ya Nyabibuye, wilaya ya Kakonko mkoani  Kigoma, ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu inayoambana na maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake ni Februari 3, mwaka huu mjini Kigoma.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua soko la Kata ya Nyabibuye, Kakonko leo Januari 30, 2013, ikiwa ni ziara ya Katibu Mkuu inayoambana na maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake ni Februari 3, mwaka huu mjini Kigoma. Kushoto ni diwani wa kata hiyo Steven Mnigakiko na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kakonko Peter Toima.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua ujenzi wa daraja la Umoja linalounganisha Kata ya Nyabibuye, Kakonko na vijiji jirani vya Burundi. alipokuwa katika ziara wilayani Kakonko mkoani Kigoma, Januari 30, mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu inayoambana na maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake ni Februari 3, mwaka huu mjini Kigoma.
 Kinana na ujumbe wake wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa daraja hilo
 Ujenzi wa daraja hilo umefikia hapa
 Maelezo ya mradi wa ujenzi wa daraja hilo
 Kinana akipanda mti kwenye shule ya sekondari ya Nyamtukuza, katika Kata ya Nyabibuye wilayani  Kakonko mkoani Kigoma. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Amani Ntibakiza
 Wanafunzi wa shule hiyo wakisomba mawe kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo, alipofika kwa ajili ya kushiriki ujenzi wa nyumba ya walimu. Pia Kinana ameahidi kuipa shule, Mashine mbili za umeme wa Solar na kompyuta.
 Kinana akiwasalimia wanafunzi wa shule hiyo



Kinana akishiriki kusomba mawe kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu katika shule hiyo

KINANA AFANYA MAMBO MAKUBWA WILAYANI KAKONKO

 Wananchi wa rika zote wa Kijiji cha Rumashi, Kata ya Nyabibuye, wilayani Kakonko, Kigoma wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahma Kinan... [Read More]

NAPE AWAPOTEZA KABISA WAPINZANI KATA YA RUNGWE JUU NA ASANTE NYERERE

Wananchi wa Rungwe Juu na  Asante Nyerere  wakishiriki kwa wingi kwenye mapokezi ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Ndugu Nape Nnauye alipo... [Read More]