Google PlusRSS FeedEmail

NAPE AWAPOTEZA KABISA WAPINZANI KATA YA RUNGWE JUU NA ASANTE NYERERE

Wananchi wa Rungwe Juu na  Asante Nyerere  wakishiriki kwa wingi kwenye mapokezi ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Ndugu Nape Nnauye alipowasili Rungwe Kata ya Asante Nyerere.

Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akipokewa kwa mapokezi makubwa ,kulia kwake ni Mjumbe wa NEC wilaya ya Kasulu,Ndugu Daniel Nswanzigwanko

Vijana wa Kata ya Asante Nyerere nao hawakuwa nyuma katika mapokezi ya kiongozi wao wa Kitaifa.Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi,Nape Moses Nnauye.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi  Nape Nnauye akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi za chama kata ya Asante Nyerere wilaya ya Rungwe.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi kata ya Asante Nyerere ,Ndugu Yohana ,akiwahutubia wananchi wa kata hiyo kwamba amerudi rasmi nyumbani,pamoja na yeye wapo wengine wengi wamerudisha kadi zao akiwemo Katibu wake Ndugu Frank Ignas Mudala,kadi zao zilirudishwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Asante Nyerere ambapo Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi alihutubia.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa wilaya ya Rungwe ,kata ya Asante Nyerere na kuwaambia wasifanye makosa katika kuchagua viongozi, wachague viongozi wenye sifa,wapenda maendeleo na wanaojali wananchi na kuelewa thamani ya amani ya nchi yetu.

This entry was posted in

Leave a Reply