Google PlusRSS FeedEmail

MSAFARA WA KINANA UNAOSAFIRI KWA TRENI DAR-KIGOMA WAFIKA TABORA JIONI HII

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akinunua mishikaki kwa mmoja wa wauzaji wa vyakula mbalimbali husuasan nyama, baada ya kuwasili na msafara wake stesheni ya Saranda, mkoani Singida, leo mchana. Kinana na msafara wake wa wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, wanasafiri kwa treni kutoka Dar es Salaam, kwenda Kigoma kwenye sherehe za miaka 36 ya CCM. (Wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Mgana Msindai. (Picha na Bashir Nkoromo)

 Makatibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kulia) na wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (wapili kulia) wakinunua chakula kwa mamalishe, kwenye stendi ya Saranda mkoani Singida, daaba ya kuwasili kwenye stesheni hiyo, Wakati Msafara wa Sekretarieti ya CCM ukiongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ulipokuwa katika safari yake kwa treni kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kwenye sherehe za miaka 36 ya CCM.(Picha na Bashir Nkoromo)
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa KImataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mstaafu John Chiligati wakishiriki kucheza ngoma ya wakazi wa mkoa wa Singida, Wakati Msafara wa Sekretarieti ya CCM ukiongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ulipokuwa katika safari yake kwa treni kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kwenye sherehe za miaka 36 ya CCM. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Martine Shigela.(Picha na Bashir Nkoromo).
  Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa KImataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akipuliza filimbi kuchangamsha ngoma aliyokuwa akishiriki kucheza na wananchi wa mkoa wa Singida, katika burudani ya ngoma iliyotolewa, Wakati Msafara wa Sekretarieti ya CCM ukiongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ulipokuwa katika safari yake kwa treni kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kwenye sherehe za miaka 36 ya CCM.(Picha na Bashir Nkoromo)

This entry was posted in

Leave a Reply