Google PlusRSS FeedEmail

WAJUMBE WA SEKRETARIETI WAWASILI SALAMA KIGOMA LEO


Dk.Asha Rose Migiro Katibu wa NEC  Siasa na Uhusiano wa Kimataifa( wa pili kulia) na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye wakiwa na furaha baada ya kuwasili Kigoma salama leo hii

Katibu wa CCM  Taifa, Ndugu Abdulrahaman Kinana akisalimiana na Daniel Nswanzigwanko mara baada ya kuwasili salama mjini Kigoma leo.

Katibu Mkuu akivishwa skafu mara tu baada ya kuwasili Kigoma leo kwa usafiri wa treni ya reli ya kati tokea Dar es salaam.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kupiga ngoma wakati wa mapokezi ya Wajumbe wa  Sekretarieti ,uliowasili leo Kigoma  kwa ajili ya sherehe za miaka 36 ya CCM.

Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahaman Kinana pamoja na wajumbe wa Sekretarieti wakitoa salaam za shukrani kwa wana Kigoma kwa mapokezi mazuri,pia Katibu Mkuu aliwaeleza wananchi wa Kigoma hiyo reli ni ya kila mtanzania hivyo tunajukumu la kuilinda na kuitunza.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa dereva wa treni Kambi Ali, wakiwa kwenye picha ya pamoja baada kuwasili mjini Kigoma leo asubuhi. Wengine kwenye picha ni wajumbe wa Sekretarieti na Viongozi wa mkoa wa Kigoma. PICHA ZOTE NA ADAM MZEE. PICHA ZAIDI BOFYA HAPA





This entry was posted in

Leave a Reply