* Ni kwa kukiri kumiliki kadi ya CCM
* Adai hiyo ni mara ya kwanza kwa Slaa kuwa mkweli.
*Amwambia sasa aache unafiki, kuongoza ni kuonyesha njia.NA BASHIR NKOROMO
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema anampongeza Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa kwa kukiri kwamba anamiliki kadi ya CCM hadi leo.
"Kwanza nampongeza kwa kuanza kujifunza kusema ukweli maishani mwake, bila shaka ametambua kuwa uongo haulipi. Kitendo cha kukiri anamiliki kadi ya CCM bado ni cha kiungwana, kwa hili nampongeza", alisema Nape, baada ya Mwandishi wetu kumtaka maoni yake juu ya Dk. Slaa kukiri kwenye vyombo vya habari kwamba anamiliki kadi ya CCM hadi sasa.
Akijibu tuhuma za Nape alizotoa juzi kwamba, baadhi ya vigogo wa Chadema akiwemo Dk. Slaa bado wana kadi za CCM na baadhi yao wanaendelea kuzilipia, Katibu huyo wa Chadema kupitia vyombo vya habari, amekiri kuwa anayo kadi ya CCM na kwamba anaitunza kama kumbukumbu muhimu kwake.
Pamoja na pongezi hizo, Nape amemtaka Dk. Slaa kuwambia Watanzania kwamba ameilipia mpaka lini kadi hiyo ya CCM na pia aache tabia ya kuwadanganya wenzake kurudisha kadi zao za CCM huku yeye akibaki na yake kibindoni.
"Ni vizuri sasa Dk. Slaa awaambie Watanzania amelipia mpaka lini kadi hii. Lakini aache kuwadanganya wenzake kurudisha kadi zao huku yeye akibaki na yake' huu ni unafiki", alisema Nape.
Aidha Nape ambaye amekiri kumheshimu sana Dk. Slaa kama Babu yake, amesema alishituka sana kusikia Katibu Mkuu huyo wa Chadema akiwatuhumu viongozi wa chama hicho, hivi karibuni kuwa ni mamluki wa CCM huku akijua yeye ni mamluki namba moja kwani wenzie hawana kadi za CCM yeye anayo.
"Nimesikia anahoji hili linawasaidiaje Watanzania masikini!? Swali hili limethibitisha upeo mdogo sana wa kufikiri wa kiongozi mkubwa na ninayemheshimu kama huyu. lazima ajue kwamba yeye anaomba kuwa kiongozi hivyo lazima wananchi tumjue tabia zake", alisema Nape na kuongeza;
"viongozi wanafiki wa aina yake ni janga kwa taifa letu.Usipokuwa mwaminifu kwa kidogo huwezi kuwa mwaminifu kwa kikubwa. lazima anayetaka kuwa kiongozi aishi anayoyasema".
Bas naona kama tulikuwa tunahesabu idadi ya wanachama wetu kwa kujumuisha watu kama Dr. Slaa na wengineo basi idadi inayotambulika ya wanachama wa CCM itakuwa na dosari kubwa sana.
Na kwa kipindi chote hicho kwa nini hatujamfukuza uanachama? Tusiendelee kulelea watu wa aina hii. Na je kuna wananchi wa kawaida wanaotambulika uanachama kwenye zaidi ya chama kimoja Tanzania?
Inatupasa kutafuta Mwafaka wa mambo kama haya.