Google PlusRSS FeedEmail

Zahanati ya Kiji cha Samaria ikiwa katika hatua nzuri za ujenzi, Zahanati hii inajengwa kwa fedha za Halmashauri kwa kushirikiana na wananchi.

Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana ,pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi  Ndugu Nape Nnauye wakishirikiana na wananchi kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Samaria.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Ndugu Esterina Kilasi . 

Kilimo Kwanza ndio njia pekee ya kutukomboa wakulima ,pichani Katibu Mkuu wa CCM akipokelewa na wakulima ambao wapo chini ya shirika  la kilimo(NADO) katika kijiji cha Igwachanya,wilaya wa Wanging'ombe mkoani Njombe
Umati wa wakazi wa wilaya ya Wanging'ombe waliojitokeza kwa wingi kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  katika ofisi za CCM wilaya hiyo ,pichani Katibu Mkuu wa CCM akiwasalimia wananchama na wapenzi wa CCM wa wilaya hiyo.

Katibu Mkuu wa CCM Taifa ,Ndugu Abdulrahman Kinana  akishiriki kuweka moja ya mizinga ya nyuki ya Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Wanging'ombe ,ambapo jumla ya mizinga 50 imewekwa na Katibu mkuu ameahidi kuongeza mizinga 25.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua mradi wa ufugaji nyuki wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM wilaya ya Wanging'ombe,mkoani Njombe.

Mradi wa ufugaji wa kisasa wa Nyuki ambao umezinduliwa rasmi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.


Katibu Mkuu wa CCM akiwasili Mlangali

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi katika ofisi ya CCM tawi la Wangamiko, Mlangali, mkoani Njombe.

Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Ndugu Nape Moses Nnauye akihutubia na wakazi wa Mlangali, wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe.



Joseph Kihongo akionyesha kadi yake ya Chadema kwa wakazi wa Mlangali na kuikabidhi kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kisha kukabidhiwa kadi ya CCM.

Umati wa wakazi wa Mlangali ukila kiapo cha kuwa wana CCM.

Katibu Mkuu wa CCM akiondoka Mlangali baada ya kufanya mkutano wa nguvu kwa wakazi wa kitongoji hicho.

Mapokezi ya aina yake kwa katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipowasili katika kata ya Luduga wilaya ya Wanging'ombe,  Mei 31 ,2013.


Oscar Mbafu (mwenye kofia) akisoma utenzi wake mahiri ambao ulizikonga nyoyo za wakazi wa Luduga, Utenzi wake huo pia utachapishwa kwenye gazeti la Uhuru  hivi karibuni.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Luduga ,wilaya ya Wanging'ombe,ambapo aliwasifia kwa kuwa wachapakazi na amewasisitiza hakuna miujiza katika suala la kuleta maendeleo.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya CCM aliyekuwa Katibu wa Jumuiya  ya Wazazi Chadema Wilaya ya wanging'ombe.



WAKAZI WA NJOMBE WASEMA HAKUNA NAFASI YA WAPINZANI

Zahanati ya Kiji cha Samaria ikiwa katika hatua nzuri za ujenzi, Zahanati hii inajengwa kwa fedha za Halmashauri kwa kushirikiana na wananch... [Read More]

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana ,akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Makete,Ndugu Josephine Matiro na viongozi wengine wa CCM wa Wilaya ya Makete na Mkoa wa Njombe kwenda nyumbani kwa mabalozi wa mashina ya CCM katikatika kijiji cha Tandala tarehe 30 Mei 2013.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa shina la Tandala ,kata ya Singida,kijiji cha Tandala,wilaya ya Makete, mkoa wa Njombe.
Balozi wa Shina la Tandala,Bi. Zakina Sanga akiwa mwenye uso wa furaha baada ya kutembelewa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa,Ndugu Abdulrahman Kinana.
Balozi Paschal Sanga wa shina la CCM  namba 8, akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM  kwenye shina hilo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa shina na 8,na kuwaambia CCM inathamini sana uwepo wa mabalozi.
Wakazi wa shina namba 8 kwa Balozi Paschal Sanga,wakishangilia hotuba ya katibu Mkuu wa CCM ,Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa , Ndugu Abdulrahman Kinana amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali wa CCM kuwa karibu na mabalozi wa mashina na kuhakikisha wanawatembelea mara kwa mara.  Katibu Mkuu alisema pia viongozi hawana budi kuongeza moyo wa kujitolea, akizungumza nyumbani kwa Balozi wa Shina la Tandala, Bi. Zakina Sanga ,alisema hakuna chama kitakachoahidi miujiza na kusisitiza kuwa CCM kimeahidi na kitahidi yale ambayo yanawezekana na kuyatimiza kwa wakati. Alisisitiza kuwa viongozi wajuu wa CCM lazima waje kwa mabalozi wa mashina maana hao ndio wenye wanachama na wanachama ndio mtaji mkubwa wa chama chetu. "Kuwa kiongozi maana yake kuwa mtumishi wa wananchi na sio kuwa mtukufu kwa wananchi."

VIONGOZI WA CCM WATAKIWA KUWA KARIBU NA MABALOZI WA MASHINA

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana ,akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Makete,Ndugu Josephine Matiro na viongozi wengine wa CCM wa Wi... [Read More]

*Akagua ufukwe wa ziwa Nyansa katika mwambao wa ziwa hilo kwenye kijiji cha Lupingu, wilayani Ludewa, na kuwambia wananchi wasihofu na maneno Malawi kuhusu ziwa hilo, Serikali ipo imara kuwalinda usiku na mchana.

*Akagua na kuimarisha uhai wa Chama ngazi za chini kabisa za matawi na mashina. Ahudhuria vikao vya mashina na wajumbe wa nyumba kumi yaliyoko ndani ndani vijijini na kufanya mikutano ya hadhara iliyojaa shamra shamra, apokea wanachama wapya kibao

*Akagua hatua zinazoendelea katika upembuzi yakinifu wa mradi wa makaa ya mawe na chuma Liganga, aahidi wanannchi kushirikishwa kwa karibu mambo yakiiva.

UKAGUZI MWAMBAO WA ZIWA NYASA
 KATIBU Mkuu wa CCM, Kanali mstaafu, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kulia) wakiwa kwenye ufukwe wa ziwa Nyasa, kwenye mwambao wa ziwa hilo katika Kijiji cha Lupingu, Kata ya Lupingu Wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe, leo Mei 29, 2013, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama na kusikiliza kero za wananchi katika mkoa huo. Wengine ni Mbunge wa Ludewa, Deo Philikunjombe na Mbunge wa Mwibala Kange Lugora.
 KATIBU Mkuu wa CCM, Kanali mstaafu, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kulia) wakiwa kwenye ufukwe wa ziwa Nyasa, kwenye mwambao wa ziwa hilo katika Kijiji cha Lupingu, Kata ya Lupingu Wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe, leo Mei 29, 2013, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama na kusikiliza kero za wananchi katika mkoa huo.
 Nape na Lugora wakieleweshana jambo kuhusu ziwa hilo
 Kinana na baadhi ya viongozi aliokuwa nao kwenye msafara wake wakiwa kwenye ufukwe wa ziwa hilo kwenye kijiji hicho, Majini ni Mbunge wa viti maalum na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Pindi Chana.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Nape wakipiga picha ya pamoja na baadhi ya walioambatana nao kwenye msafara huo.
 Monica Msemwa akimuogesha mtoto kwenye ufukwe wa ziwa hilo la Nyasa. katika kijiji cha Lupingu wilayani Ludewa mkoani Njomba.
Kinana na msafara wake wakipita kwenye mitaa ya kijiji hicho cha Lupingu baada ya kukagua ufukwe wa ziwa Nyasa. (Pichzote na BASHIR NKOROMO)

KUKAGUA NA KUIMARISHA UHAI WA CHAMA NGAZI ZA CHINI KABISA
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza katika kikao cha shila  namba moja, tawi la Lupingu, Wilaya ya Ludewa. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Pindi Chana, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga au 'Jah People'
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia mwananchi aliyekuwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha wavuvi cha Lupingu, wilayani Ludewa
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpa kadi ya uanachama wa CCM, Flowin Mkinga, katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Lupingu. Jumla ya wanachama wapya 32 walipata kadi za CCM.
 Wanachama wapya waliopewa kadi wakila kiapo. Kulia ni Kinana akishiriki kwenye kiapo hicho cha utii kwa CCM
 Msanii akiikung'uta ngoma kwa maarifa yake yote, wakati kikundi cha ngoma ya mng'anda kilipotumbuiza kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kijiji cha Lupingu.
Wasanii wa ngoma ya mng'anda wakionyesha uhodari bwa kucheza ngoma hiyo, kwneye mkutano wa hatadhara uliofanyika katika kijiji cha Lupingu. (Picha zote na BASHIR NKOROMO

  • MCHUCHUMA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) akionyeshwa sampuli mbalimbali za madini ya chuma kwenye kituo kinachofanya utafiti wa awali kuhusu kiwango cha chuma kinachoweza kupatikana kwa kuchimbwa eneo la Liganga, wilayani Ludewa mkoani Njombe alipotembelea karakana ya kampuni ya Kichina ya Tanzania China International Mineral Resorce Ltd, inayofanya uchunguzi huo. Anayempa maelezo ni  Meneja Utawala wa kampuni hiyo, Tao Jian. Kushoto ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) akionyeshwa sampuli mbalimbali za madini ya chuma kwenye kituo kinachofanya utafiti wa awali kuhusu kiwango cha chuma kinachoweza kupatikana kwa kuchimbwa eneo la Liganga, wilayani Ludewa mkoani Njombe alipotembelea karakana ya kampuni ya Kichina ya Tanzania China International Mineral Resorce Ltd, inayofanya uchunguzi huo. Anayempa maelezo ni  Meneja Utawala wa kampuni hiyo, Tao Jian.
 Tao Jian akiwaonyesha Kinana na msafara wake, ramani linalofanyiwa kazi na kampuni yake katika kutafiti aina na kiasi cha Chuma kitakachoweza kupatikana Liganga
 Mabosi wa Kampuni ya Kichina inayofanya utafiti wa aina na kiasi cha chuma kitakachopatikana Liganga, wakitoa maelezo ya jumla kuhusu mradi huo unavyoendelea
Kilima cha madini ya Chuma, kinavyoonekana kwa mbali eneo la Liganga PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

ZIARA YA KINANA, NAPE YATIKISA MKOANI NJOMBE

*Akagua ufukwe wa ziwa Nyansa katika mwambao wa ziwa hilo kwenye kijiji cha Lupingu, wilayani Ludewa, na kuwambia wananchi wasihofu na manen... [Read More]

Mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Ndg. Mattar Zahran Said akihutubia Wananchi na Wanaccm na kujidani huku akiomba ridhaa ya wananchi wamchague ili wakiwawakilishe Bungeni katika Mkutano wa hadhara uliofanywa katika viwanja vya Skuli ya Ukutini Jimboni humo.

Mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Ndg. Mattar Zahran Said akihutubia Wananchi na Wanaccm na kujidani huku akiomba ridhaa y... [Read More]

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe: Balozi Seif Ali Iddi akimtambulisha Mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya CCM wa Jimbo la Chambani Ndg. Mattar Zahran Said katika Mkutano wa hadhara uliofanyika siku ya tarehe 26/05/2013 katika viwanja vya Skuli ya Ukutini Jimboni humo.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe: Balozi Seif Ali Iddi akimtambulisha Mgombea wa Ubunge kwa... [Read More]

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mgombea wa CCM wa Kiti ch... [Read More]

Mgeni rasmi Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia Wanaccm na Wananchi wa Jimbo la Chambani wakati wa Mkutano wa Hadhara katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo hilo.

Mgeni rasmi Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia Wanaccm na Wananchi wa Jimbo la Chambani wakati wa Mkutano wa Hadhara katika kampeni za u... [Read More]

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Mhe Vuai Ali Vuai akimkaribisha Mgeni Rasmi wakati wa Kampeni za Uzinduzi wa uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Chambani.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Mhe Vuai Ali Vuai akimkaribisha Mgeni Rasmi wakati wa Kampeni za Uzinduzi wa uchaguzi mdogo wa Ubunge kat... [Read More]

Vijana wakisoma Utenzi mbele ya Mgeni rasmi, wakati wa mkutano wa hadhara katika uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Chambani Mkoani Pemba.

Vijana wakisoma Utenzi mbele ya Mgeni rasmi, wakati wa mkutano wa hadhara katika uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Jimbo la... [Read More]

Umati mkubwa wa Wanaccm na Wananchi wa Jimbo la Chambani wakimsikiliza Mgeni Rasmi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe: Balozi Seif Iddi ambae hayupo pichani katika mkutano wa hadhara wa Uzinduzi wa Kampeni wa uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Jimbo hilo.

Umati mkubwa wa Wanaccm na Wananchi wa Jimbo la Chambani wakimsikiliza Mgeni Rasmi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Pia ni Makamu wa Pili wa ... [Read More]


WanaCCM na Wananchi wa Jimbo la Chambani Wakimsiliza Mgeni Rasmi wakati akiuhutubia Umma katika mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi mdogo wa Kiti cha Ubunge Jimbo la Chambani Mkoani Pemba.

KAMPENI ZA CCM KUGOMBEA KITI CHA UBUNGE KATIKA UCHAGUZI MDOGO WA JIMBO LA CHAMBANI ZAZINDULIWA RASMI NA MHE. BLZ SEIF ALI IDDI MJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM AMBAE PIA NI MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR, TAREHE 26/05/2013.

WanaCCM na Wananchi wa Jimbo la Chambani Wakimsiliza Mgeni Rasmi wakati akiuhutubia Umma katika mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa Kampeni za... [Read More]