Na Ali Mwunyu Msuko
Zanzibar
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein anaendelea na ziara yake ya kichama kwa kuutembelea Mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo jana tarehe 2/5/2013 aliitembelea Wilaya ya Kaskszini "A".
Alipofika Wilayani humo katika kijiji cha Moga. Dr. Shein aliweka Jiwe la Msingi la Maskan ya Dr. Salmin na kusalimiana na wan CCM na wananchi wa Moga.
Mnamo saa 5.30 Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar aliwasili kwenye kijiji cha Kijini na kuweka Jiwe la Mshingi kwenye jengo la Ofisi ya CCM ya Tawi la Kijini.
Baadae Dr. Shein alifika Bwereu na kuweka jiwe la Msingi Jengo la Ofisi ya CCM ya Tawi la Bwereu. Akiendelea na ziara yake hiyo pia alifika katika kijiji cha Kidoti, ambapo hapo aliweka jiwe la Msingi katika jengo la Madrasa ya Quran. Hapo hapo Kidoti alikaguwa Darasa la Itikadi la wanachama wa CCM na luwakabidhi kadi wanachama wapya wasiopungua 100.
Mnamo saa 9.00 alaasiri Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar aliwasili katika kijiji cha Nungwi na kufanya kazi ya kuweka Juwe la Msingi Maskani ya Msuguri na katika Maskani hiyo alizindua rasmi kikundi cha Ushirika wa Ushoni cha Maskani hiyo.
Baada ya kuondoka Maskan ya Msuguri alikwenda kwenye Maskani ya Amani na Utulivu katika Kijiji hicho hicho cha Nugwi na Kweka Jiwe la Msingi la Maskani hiyo na baadae kufanya kazi ya kuwapokea wanachama 50 wa Chama cha CUF ambao waliamua kwa hiyari yao kukihama chama hicho na kujiunga na CCM, pia aliwakabidhi kadi wanachama wapya wa CCM 250.
Mwisho Dr. Shein alipata nafasi ya kusalimiana na wana CCM na wananchi wa Nungwi.
Dr. Shein anaendelea na ziara yake kwa kuitembelea Wilaya ya Kaskazini "B" leo.