Google PlusRSS FeedEmail

KINANA AWASILI NJOMBE TAYARI KWA ZIARA YA SIKU SABA

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akilakiwa na Mbunge wa Njombe Kaskazini,Mh Deo Sanga a.k.a Jah People mara baada ya kuwasili jioni ya leo mpakani mwa Mkoa wa Iringa na Njombe katika kijiji cha Idofi,kata ya Mlowa,ambapo pia alipokelewa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Njombe akitokea Mkoani Iringa ambaka aliwasili leo Asubuhi akitokea jijini Dar akiwa ameambatana na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye.

Ndugu Kinana na ujumbe wake watakuwa na ziara na ziara ya siku saba mkoani Njombe ambapo watatembele Wilaya zote za Njombe,Makete, Ludewa na Wanging'ombe  wakiimarisha chama na kusikiliza matatizo ya Wananchi,huku wakikagua miradi ya maendeleo mbalimbali katika kusimamia serikali ili kutekeleza Ilani uchaguzi ya CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akivalishwa skafu .
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Ludewa,Mh.Deo Filikunjombe,kushoto shati la drafti ni Mbunge wa jimbo la Mwibara,Mh Kange Rugora


Pichani kulia ni Mjumbe wa kamati kuu na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Njombe,Pindi Chana akicheza na akina mama wakati wa mapokezi ya katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana 
 Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye  akishirikiana na  mmoja wa wapiga ngoma za asili wakati walipowasili leo mapema mchana wakiongozwa na  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana
 Ndugu Kinana na ujumbe wake wakipokelewa kwa shangwe mapema jionu ya leo,mpakani mwa Mkoa wa Iringa na Njombe katika kijiji cha Idofi,kata ya Mlowa,ambapo pia alipokelewa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Njombe akitokea Mkoani Iringa ambaka aliwasili leo Asubuhi akitokea jijini Dar akiwa ameambatana na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye .
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akitazama moja ya kikundi cha ngoma kilichofika kumlaki,mara baada ya kuwasili jioni ya leo mpakani mwa Mkoa wa Iringa na Njombe katika kijiji cha Idofi,kata ya Mlowa,ambapo pia alipokelewa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Njombe akitokea Mkoani Iringa ambaka aliwasili leo Asubuhi akitokea jijini Dar akiwa ameambatana na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye.


This entry was posted in

Leave a Reply