Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi, akizungumza wakati wa Mkutano wa 12 wa Masuala ya Wazawa, kuhusu mada ya utafiti uliofanywa kuhusu Ujasiri, Maarifa ya Jadi na Kujenga uwezo Jamii ya Wafugaji katika Afrika. Nyuma ya Balozi ni Bi. Ellen Maduhu Afisa wa Ubalozi .
NA MWANDISHI MAALUM, NEW YORK
Tanzania imesisitiza kwamba inajukumu kubwa la kuhakikisha kuwa mipango yake ya maendeleo endelevu inamfikia kila mwananchi na kwamba hakuna jamii itakayo achwa nyuma.
Na kwa sababu hiyo, Tanzania imeitaka Jumuiya ya Kimataifa na wadau wengine kushirikiana na Serikali katika kufanikisha azma yake hiyo, lakini pia kutambua kuwa maamuzi mbalimbali inayoyachukua yanafanyika kwa nia njema.
Hayo yameelezwa na Balozi Ramadhan Mwinyi, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, alipokuwa akichangia majadiliano ya mada ya utafiti kuhusu Ujasiri, Maarifa ya Jadi na Kujenga Uwezo wa Jamii ya Wafugaji katika Afrika.
Mada hiyo ni sehemu ya mada kadhaa zikiwa zao afya, elimu, haki za binadamu, ujasiliamali, vijana mila na tamadu ambazo zimekuwa zikijadiliwa kwa nyakati tofauti katika Mkutano wa Kudumu wa 12 Kuhusu Masuala ya Wazawa. ( Forum on Indigenous Issues) Mkutano huu ambao ulianza mapema wiki hii unafanyika chini ya usimamizi wa Baraza la Uchumi na Maendeleo ya Jamii la Umoja wa Mataifa ( ECOSOC).
Washiriki wa mkutano huu wapatao 2000 wanatoka katika Asasi zisizo za kiserikali wakiwamo wawakilishi kutoka baadhi ya taasisi za kifedha kama Banki ya Dunia, Banki ya Maendeleo ya Afrika na Banki ya Maendeleo ya Asia.
“Tunaendelea na jitihada za kuwaletea maendeleo wananchi wetu ili kuhakikisha kwamba hakuna jamii inayoachwa nyuma kama ambavyo imeainishwa katika Malengo ya Maendeleo ya Millenia ( MDGs) na kutafsriwa katika Mpango wa Maendeleo ya Taifa na mipango migineyo” akasisitiza Balozi Mwinyi.
Hata hivyo akasema licha ya jitihada hizo za serikali , bado kuna baadhi ya jamii chache ambazo zenyewe zimeamua kudumisha mila, tamaduni na maisha yao ya jadi .
Akasema jamii hizo ni zile ambazo hazifahamiki sana katika Jumuiya ya Kimataifa kama ilivyo kwa jamii ya wamasaai.
Akizungumzia masuala ya upatikanaji na ugawaji wa ardhi kwa wananchi zikiwamo jamii ambazo mfumo wa maisha yao unategemea zaidi ardhi na mali asili nyingine. Balozi Mwinyi amewaeleza washiriki wa mkutano huo wakiwamo washiriki kutoka Tanzania, kwamba serikali imejiwekea sheria na taratibu zinazosimamia ugawaji wa ardhi.
Akafafanua kwa kueleza kwamba kwa sheria na taratibu za Tanzania, Hati ya umiliki wa Ardhi katika ngazi ya kijiji hutolewa kwa wanajamii ambao wanaishi au wamekusanyika katika muundo wa kijiji ambao unatambuliwa rasmi.
“ Kwa mujibu wa sheria zetu, ni kijiji ndicho kinatambuliwa kisheria kama chombo huru kinachosimamia masuala ya ardhi ambapo cheti cha ardhi hutolewa kwaajili ya matumizi ya jamii nzima”. Akasema
Na kuongea “ Hata hivyo kuna baadhi ya maeneo hasa yale ya wawindaji ambapo kama idadi ya jamii ile haikukidhi matakwa ya kisheria ya kuwa na hadhi ya kijiji kutokana na uchache wao, bado kwa mfano, mwaka 2011, serikali ilitoa hati ya kumiliki ardhi kwa ya Wahdzabe ingawa walikosa sifa zinazotakiwa kisheria.
Akizungumza kuhusu Loliondo ambako Serikali imetangaza kutenga eneo la kiasi cha kilomita za mraba 2,500 za ardhi kwaajili ya makazi ya jamii ya wamasaai na ambao wengi wao hawakuwa na ardhi na hivyo kuwa katika mazingira magumu. Balozi amesisitiza kwamba uamuzi huo ulikuwa ni wa manufaa kwa jamii hiyo na taifa kwa ujumla.
Akasema kuwa eneo lililotengwa ni kubwa kuliko nchi ya Luxeburg au mara nne ya eneo la nchi ya Singapore ambayo ina kilomita za mraba 624.
Akasema eneo lililobaki la kilomita za mraba 1,500 Serikali imelitenga kwaajili ya hifadhi ya wanyama pori na mazalia yake ikiwa ni pamoja na uhifadhi wa uoto wa asili, utunzaji wa vyanzo vya maji kwa maendeleo endelevu ya uwepo wa wanyama na kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Naibu Mwakilishi wa Kudumu akafafanua Zaidi kwa kueleza kwamba, uamuzi huu wa Serikali wa kutenga ardhi kwaajili ya matumizi ya binadamu na mengine kwa hifadhi ya maliasili ni uamuzi halali na wala haukuanza sasa bali umekuwa ukitekelezwa katika maeneo mengi ya nchi tangu uhuru.
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
-
▼
2013
(633)
-
▼
May
(74)
- WAKAZI WA NJOMBE WASEMA HAKUNA NAFASI YA WAPINZANI
- VIONGOZI WA CCM WATAKIWA KUWA KARIBU NA MABALOZI W...
- ZIARA YA KINANA, NAPE YATIKISA MKOANI NJOMBE
- Mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduz...
- Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM ambaye pia ni Makamu w...
- Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Pi...
- Mgeni rasmi Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia...
- Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Mhe Vuai Ali Vu...
- Vijana wakisoma Utenzi mbele ya Mgeni rasmi, wakat...
- Umati mkubwa wa Wanaccm na Wananchi wa Jimbo la Ch...
- KAMPENI ZA CCM KUGOMBEA KITI CHA UBUNGE KATIKA UCH...
- KINANA KUHUTUBIA WANANCHI WA LUDEWA LEO
- KINANA AWASILI NJOMBE TAYARI KWA ZIARA YA SIKU SABA
- KINANA, NAPE WATUA IRINGA TAYARI KWA ZIARA KAZI M...
- HAKUNA JAMII ITAKAYOACHWA NYUMA KIMAENDELEO: TAN...
- NAPE NDANI YA MIAKA 150 YA SPD
- DK. ASHA-ROSE ATAJA MAAZIMIO YA KIKAO CHA KAMATI K...
- PRESS RELEASE
- MWENYEKITI WA CCM, RAIS KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA ...
- CCM YATOA ONYO KWA WANAOJIPITISHA PITISHA NA KUJIT...
- TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
- RAIS KIKWETE AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KATIKA ...
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHANI MSIBA WA ALLY SYKE...
- MWENYEKITI WA CCM, RAIS KIKWETE AFANYA KIKAO MUHIM...
- RAIS KIKWETE AZINDUA KAMPENI YA LISHE LEO
- UNESCO YAENDESHA WARSHA KUHUSU RIPOTI YA HALI YA E...
- CCM YAWAPONGEZA VIONGOZI WA DINI
- MKURUGENZI WA FES NCHINI AIPONGEZA CCM KWA KUJENGA...
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MCHUNGAJI DKT...
- RAIS KIKWETE AZINDUA JENGO LA SAYANSI KATIKA KITUO...
- WATANZANIA WENGI JIJI LA CARDIFF-WALES (UK) WAJIUN...
- NAPE AMWAGIZA DC IGUNGA KUSIMAMIA KWA IUMARA UTEKE...
- MPOKEZI YA DK. KAFUMU IGUNGA YAFUNIKA
- CCM MAMBO SAFI, MAHAKAMA KUU YAMREJESHEA UBUNGE DK...
- CCM YALAANI VIKALI SHAMBULIO LA BOMU ARUSHA
- RAIS KIKWETE AKATIZA ZIARA YA KUWAIT KUFUATIA SHAM...
- BALOZI WA SUDANI NCHINI AMTEMBELEA MANGULA LEO
- CHADEMA HOI MBEYA
- NAPE: CHADEMA WANAUGUA KIFAFA CHA SIASA
- TAMKO LA RAIS JUU YA TUKIO LA ARUSHA
- TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
- RAIS KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA BALOZI TANDAU, DAR
- Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe. Dk. Ali Moh...
- Wanachama wa CCM na Wananchi wa Kijiji cha Nungwi ...
- Mmmoja kati ya vijana 50 waliokuwa Wanachama wa CU...
- Dr. Shein akimkabidhi Kadi ya CCM mwnachama mpya w...
- Dr. Shein aangalia shughuli za ushoni zinazofanywa...
- MakamuMwnyekiti wa CCM Zanzibar akikata utepe kuon...
- Dr. Shein akiweka jiwe la Msingi Maskani ya Msugur...
- Wana CCM na wananchi wa Kidoti wakimsikiliza kwa m...
- Wana Madrasa wakishangilia kwa kupiga Dufu wakati ...
- RAIS KIKWETE AFARIJI FAMILIA YA MAREHEMU MZEE ALFR...
- KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI OMBENI SEFUE AKUTANA N...
- RAIS ALIPOHUTUBIA SIKU YA MEI MOSI
- Mkamu Mwenykiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanziba...
- Wnachama wapya wa CCM wakila kiapo baada ya kukabi...
- Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dr Ali Mohammed ...
- Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanziba akimkabidhi kadi ...
- Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akiziangalia kad...
- WanaCCM na wananchi wakimsikiliza kwa makini Makam...
- Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dr. Ali Muhamed ...
- Wana CCM wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Z...
- Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Akiweka mlingoti...
- Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dr. Ali Mohammed...
- RAIS KIKWETE AONGOZA SHEREHE ZA MEI MOSI MBEYA
- Vijana wa CCM Wakisoma Utenzi mbele ya Makamu Mwen...
- Vijana wa Big Star Ngoma wakitumbuiza katika Mkuta...
- No title
- No title
- No title
- Dr.Shein asema kazi imeanza CCM.
- Dr.Shein akifungua Tawi la CCM ni moja kati ya zia...
- Dr.Shein akivishwa skafu na chipkizi wa CCM wakati...
- Dr.Shein afanya ziara ya kichama kutembelea Mikoa ...
-
▼
May
(74)
LOVE LINKS
Powered by Blogger.