Google PlusRSS FeedEmail

KINANA KUHUTUBIA WANANCHI WA LUDEWA LEO

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,akifahamishwa jambo na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe,Deo Sanga,kushoto ni Katibu wa Uchumi na Fedha Ndugu Clemence Malekela.
Katibu Mkuu wa CCM ,Ndugu Abdulrahman Kinana leo atahutubia wananchi wa Ludewa,mkoani Njombe.Akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye,Katibu Mkuu anatarajiwa kuanza safari asubuhi hii akitokea Njombe mjini kuelekea Malangali ambapo atasomewa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM. Baadae atawatembelea mabalozi wawili wa mashina ya CCM,Katibu Mkuu atahutubia mkutano wa hadhara Mawengi na kuelekea Ludewa mjini ambapo atafanya kikao na wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya na kuhitimisha kwa mkutano wa hadhara.

This entry was posted in

Leave a Reply