Google PlusRSS FeedEmail

VIONGOZI WA CCM WATAKIWA KUWA KARIBU NA MABALOZI WA MASHINA

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana ,akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Makete,Ndugu Josephine Matiro na viongozi wengine wa CCM wa Wilaya ya Makete na Mkoa wa Njombe kwenda nyumbani kwa mabalozi wa mashina ya CCM katikatika kijiji cha Tandala tarehe 30 Mei 2013.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa shina la Tandala ,kata ya Singida,kijiji cha Tandala,wilaya ya Makete, mkoa wa Njombe.
Balozi wa Shina la Tandala,Bi. Zakina Sanga akiwa mwenye uso wa furaha baada ya kutembelewa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa,Ndugu Abdulrahman Kinana.
Balozi Paschal Sanga wa shina la CCM  namba 8, akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM  kwenye shina hilo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa shina na 8,na kuwaambia CCM inathamini sana uwepo wa mabalozi.
Wakazi wa shina namba 8 kwa Balozi Paschal Sanga,wakishangilia hotuba ya katibu Mkuu wa CCM ,Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa , Ndugu Abdulrahman Kinana amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali wa CCM kuwa karibu na mabalozi wa mashina na kuhakikisha wanawatembelea mara kwa mara.  Katibu Mkuu alisema pia viongozi hawana budi kuongeza moyo wa kujitolea, akizungumza nyumbani kwa Balozi wa Shina la Tandala, Bi. Zakina Sanga ,alisema hakuna chama kitakachoahidi miujiza na kusisitiza kuwa CCM kimeahidi na kitahidi yale ambayo yanawezekana na kuyatimiza kwa wakati. Alisisitiza kuwa viongozi wajuu wa CCM lazima waje kwa mabalozi wa mashina maana hao ndio wenye wanachama na wanachama ndio mtaji mkubwa wa chama chetu. "Kuwa kiongozi maana yake kuwa mtumishi wa wananchi na sio kuwa mtukufu kwa wananchi."

This entry was posted in

Leave a Reply