Zahanati ya Kiji cha Samaria ikiwa katika hatua nzuri za ujenzi, Zahanati hii inajengwa kwa fedha za Halmashauri kwa kushirikiana na wananchi. |
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Ndugu Esterina Kilasi . |
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua mradi wa ufugaji nyuki wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM wilaya ya Wanging'ombe,mkoani Njombe. |
Mradi wa ufugaji wa kisasa wa Nyuki ambao umezinduliwa rasmi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. |
Katibu Mkuu wa CCM akiwasili Mlangali |
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi katika ofisi ya CCM tawi la Wangamiko, Mlangali, mkoani Njombe. |
Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Ndugu Nape Moses Nnauye akihutubia na wakazi wa Mlangali, wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe. |
Joseph Kihongo akionyesha kadi yake ya Chadema kwa wakazi wa Mlangali na kuikabidhi kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kisha kukabidhiwa kadi ya CCM. |
Umati wa wakazi wa Mlangali ukila kiapo cha kuwa wana CCM. |
Katibu Mkuu wa CCM akiondoka Mlangali baada ya kufanya mkutano wa nguvu kwa wakazi wa kitongoji hicho. |
Mapokezi ya aina yake kwa katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipowasili katika kata ya Luduga wilaya ya Wanging'ombe, Mei 31 ,2013. |
Oscar Mbafu (mwenye kofia) akisoma utenzi wake mahiri ambao ulizikonga nyoyo za wakazi wa Luduga, Utenzi wake huo pia utachapishwa kwenye gazeti la Uhuru hivi karibuni. |
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya CCM aliyekuwa Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Chadema Wilaya ya wanging'ombe. |