Google PlusRSS FeedEmail

KATIBU MKUU WA CHAMA CHA PPRD AWASILI KIGOMA LEO.

Katibu Mkuu wa Chama Cha PPRD ,Evarist  Bushabe ( Kulia) akisalimiana na Katibu Mwenezi  wa Chama chake  Emmanuel Embaswa mara baada ya kuwa... [Read More]

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara aliofanya leo jioni mjini Kibondo siku ya mwisho ya ziara yake wilayani humo ambayo ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambazo kilele chake kitafanyika Jumapili hii, kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara aliofanya leo jioni mjini Kibondo siku ya mwisho ya ziara yake wilayani humo ambayo ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambazo kilele chake kitafanyika Jumapili hii, kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma
Wananchi wenye shauku ya kumsikiliza Kinana wakiwa kwenye mkutano huo
 Yohana Kabwe kutoka Chadema akipokewa na Kinana kurudi CCM, wakati wa mkutano huo
 Mmoja wa vijana ambao ni wanachama wapya wa CCM waliokabidhiwa kadi na Kinana kwenye mkutano huo akifurahia kupata kadi hiyo wakati anaondoka jukwaani baada ya kukabidhiwa
 Wanachama wapya wa CCM wakiwemo wa kutoka Chadema na NCCR Mageuzi, wakila kiapo baada ya kukabidhiwa kadi na Kinana kwenye mkutano huo. Wanachama 45 walipewa kadi.
 Baadhi ya wananchi wakiwa wameamua kwenda kukaa kwenye magogo  waweze kumuona vizuri Kinana wakati akihutubia mkutano huo
 Kinana akimtuza kijana wa kikundi cha Wize Boyz cha Kibondo kundi hilo lilipotumbuiza kwemnye mkutano huo.
 Kinana wa kundi la Kibondo Comedy akionyesha machejo ya sarakasi mbele ya wananchi wakati wa mkutano huo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akimkabidhi kijana wa kundi la muziki wa Bongo Fleva, mbuzi ambaye alimnunua kwa sh.milioni 3, kwenye mnada aliofanya kwa ajili kupata fedha za kupeleka shule watoto wa wazazi kumi wasio na uwezo katika Wilaya ya Kibondo ambao wameshajitokeza. Mbuzi huyo ametolewa na Mkuu wa wilaya hiyo, Venance Mwamoto. (PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO)

KINANA AFUNGA KAZI KIBONDO KWA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA LEO

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara aliofanya leo jioni mjini Kibondo siku ya mw... [Read More]

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM BARA AWASILI KIGOMA LEO.

Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Ndugu philip Mangula akiteremka kutoka kwenye ndege ya shirika la ndege la Tanzania (Air Tanzania) ,kwenye uw... [Read More]

Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kilelema kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wa Ziara yake ya kutembelea maeneo hayo na kuweza kujionea changamoto mbali mbali wanazokabiliana nazo wananchi hao ikiwa ni pamoja na kutembelea eneo lililotengwa kwa ajili ya Ujenzi wa Soko la Kimataifa litakalowanufaisha wakazi wengi wa wilaya hiyo ambao wako kando kando ya Mto Maragarasi unaopakana na nchi jirani ya Burundi.Dkt. Migiro pia amewaasa wananchi wa maeneo hayo kuwa na umoja,mshikamano na upendo ili kuweza kuhimarisha mambo mbali mbali ya Wilaya.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akihutubia Mkutano wa hadhara kwenye Kijiji cha Buhigwe ambapo ndipo yalipo makao makuu ya Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wa Ziara yake ya kutembelea wilaya hiyo jana.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akicheza ngoma ya asili ya kabila la Waha waliokuja kumpokea.
Wananchi wa Kijiji cha Buhigwe wakimuaga Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Viongozi mbali mbali wa CCM katika Kijiji cha Mnanila,Wilayani Buhigwe.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Mnanila kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati akiendelea na Ziara yake ya kutembelea Kata zote zilizopo wilayani humo.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Buhigwe ambapo ndipo yalipo makao makuu ya Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wa Ziara yake ya kutembelea wilaya hiyo jana.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwapungia watoto wa Kijiji cha Kilelema kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma mara baada ya kumaliza kuwahutubia wananchi wa Kijiji hicho jana.
Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Buhigwe ambapo ndipo yalipo makao makuu ya Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wakimsikiliza Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro aliekuwa kwenye Ziara ya kutembelea wilaya hiyo jana.
Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe,Ndg. Gishuli Mbegesi (kulia) akikabidhi Taarifa ya Utekelezani wa Ilani ya Uchaguzi kwa Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akipokea ripoti ya Chama Wilaya ya Buhigwe,kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Buhigwe,Bi. Bennosa Mjema.Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo,Ndg. Elisha Bagwanya
Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Buhigwe wakimsikiliza Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro aliekuwa kwenye Ziara ya kutembelea wilaya hiyo jana.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akicheza ngoma ya asili ya kabila la Waha sambamba na Bibi Buchiro Edmas Kapina wakati wa Ziara ya kutembelea wilaya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma jana.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akilakiwa kwa shangwe na kinamama wa Kijiji cha Kilelema.
Mjumbe wa Halmashauri ya Kijiji cha Kilelema,Everist Samson akisoma taarifa ya kijiji kuhusiana na changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi wa kijiji hizo zikiwemo zile za kuvamiwa na majambazi wanaotoka nchi jirani ya Burundi.Kijiji hiki kipo mpakani kabisa mwa Tanzania na Burundi kwa kijiji cha Buhema Mkoani Lutana,nchini Burundi.

Wananchi wa Kijiji cha Kilelema kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakimsikiliza kwa makini Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro (hayupo pichani).
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kilelema,Benedict Samson Mahuta (kulia) akitoa ufafanuzi juu ya eneo la Soko kwa Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro (katikati),alietembelea eneo litakalojengwa soko la Kimataifa katika Kijiji hicho cha Kilelema.
Picha ya Pamoja na Watendaji wa Kijiji cha Kilelema.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro (pili kulia) akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe,Ndg. Gishuli Mbegesi Charles (kushoto) kuelekea kwenye eneo la mpaka wa Tanzania na Burundi unaotenganishwa na sehemu ya Mto Malagarasi.

MATUKIO MBALI MBALI YA ZIARA YA DK.MIGIRO ,KATIKA WILAYA MPYA YA BUHIGWE

Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kilelema kilichopo kwenye Wilaya Mpya... [Read More]

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akishiriki ujenzi wa chumba cha darasa katika shule ya sekondari Kumwambo, Wilayani Kibondo, Januari 31, 2013, ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake kitafanyika  Februari 3, 2013 kwenye Uwanja wa Lake tanganyika mjini Kigoma. Wengine ni badhi ya viongozi waliokuwa kwenye msafara wake, Mwenyekiti wa  Wazazi Tanzania, Abdallah Bulembo (aliyebeba tofali) na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dk. Amani Kaborou. (Picha na Bashir Nkoromo).

 Baadhi ya wazee, watendaji na wajumbe wa mashina wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (hayupo pichani) alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Maendeleo wa Kibondo, Januari 31, 2013, ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake kitafanyika  Februari 3, 2013 kwenye Uwanja wa Lake tanganyika mjini Kigoma. (Picha na Bashir Nkoromo).

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwaaga wananchi wa Kijiji cha  Bunyambo Wilayani Kibondo, Januari 31, 2013, ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake kitafanyika  Februari 3, 2013 kwenye Uwanja wa Lake tanganyika mjini Kigoma. Wangine ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dk. Amani Kaborou na badhi ya viongozi waliokuwa kwenye msafara wake (Picha na Bashir Nkoromo).


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) na msafara wake, wakinunua miwa njiani baada ya kukutana na muuzaji wa miwa hiyo, wakati wakitembea kwa mguu zaidi ya kilometa moja kwenda kwenye mkutano wa hadhara Kijiji cha Bunyambo, baada ya kushiriki shughuli za ujnezi wa Ofisi ya CCM katika kijiji hicho, Wilayani Kibondo, Januari 31, 2013, ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake kitafanyika  Februari 3, 2013 kwenye Uwanja wa Lake tanganyika mjini Kigoma.(Picha na Bashir Nkoromo).


KINANA ASHIRIKI KAZI ZA JAMII KIBONDO

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akishiriki ujenzi wa chumba cha darasa katika shule ya sekondari Kumwambo, Wilayani Kibond... [Read More]