Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara aliofanya leo jioni mjini Kibondo siku ya mwisho ya ziara yake wilayani humo ambayo ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambazo kilele chake kitafanyika Jumapili hii, kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma
Wananchi wenye shauku ya kumsikiliza Kinana wakiwa kwenye mkutano huoYohana Kabwe kutoka Chadema akipokewa na Kinana kurudi CCM, wakati wa mkutano huo
Mmoja wa vijana ambao ni wanachama wapya wa CCM waliokabidhiwa kadi na Kinana kwenye mkutano huo akifurahia kupata kadi hiyo wakati anaondoka jukwaani baada ya kukabidhiwa
Wanachama wapya wa CCM wakiwemo wa kutoka Chadema na NCCR Mageuzi, wakila kiapo baada ya kukabidhiwa kadi na Kinana kwenye mkutano huo. Wanachama 45 walipewa kadi.
Baadhi ya wananchi wakiwa wameamua kwenda kukaa kwenye magogo waweze kumuona vizuri Kinana wakati akihutubia mkutano huo
Kinana akimtuza kijana wa kikundi cha Wize Boyz cha Kibondo kundi hilo lilipotumbuiza kwemnye mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akimkabidhi kijana wa kundi la muziki wa Bongo Fleva, mbuzi ambaye alimnunua kwa sh.milioni 3, kwenye mnada aliofanya kwa ajili kupata fedha za kupeleka shule watoto wa wazazi kumi wasio na uwezo katika Wilaya ya Kibondo ambao wameshajitokeza. Mbuzi huyo ametolewa na Mkuu wa wilaya hiyo, Venance Mwamoto. (PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO)