Dodoma
Pamoja na hayo Baraza Kuu limefanya Uteuzi wa Baraza la wadhamini wa Jumuiya Hiyo, ambapo Baraza Kuu limewateuwa;
- Mhe. Dr Emmanuel Nchimbi (Mb)(MCC)
- Mhe. Machano Othman Said (MNEC)
- Mhe. William V. Lukuvi (Mb)(MCC)
- Mhe. Janeth Mbene (Mb) (MNEC)
- Mhe. Hamad Y. H Masaun (Mb) (MNEC)
- Mhe. Prof Anna Tibaijuka (Mb) (MCC)
- Mhe. Mohamed Abood (MNEC)
Ambapo Baraza Kuu pia limemteua Mhe. Dr Emmanuel Nchimbi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini.
Lakini pia Baraza Kuu limefanya Uteuzi wa Kamati ya Utekelezaji ambapo wajumbe kumi (10) wameteuliwa watano (5) kutoka bara na watano (5) kutoka Zanzibar, ambao ni;
Kutoka Bara.
- Ndugu. Seki Kasida
- Ndugu Amir A Mkalipa
- Ndugu Reuben Sixbert
- Ndugu Maryam Chaurembo
- Ndugu Daudi Njaru
Kutoka Zanzibar.
- Ndugu Bakari Mussa
- Ndugu Viwe Khamis
- Ndugu Nadra J. Mohamed
- Ndugu Shaka Abdu Shaka
- Ndugu Ally Juma Nassoro
Pamoja na mijadala hiyo ya kuimarisha jumuiya ya Vijana, pia Baraza Kuu la UVCCM Taifa limetoa Maazimio yafuatayo;
- Jumuiya iendelee kuwa mtetezi wa wanyonge.
- Kutafuta na kutenga maeneo ya kilimo na kufungua mashamba ili kuiunga mkono sera ya Taifa ya Kilimo kwanza na kuwa chanzo cha mapato.
- Kuwepo na ufafanuzi wa kutosha kwa wananchi juu ya mgawanyo wa rasilimali za Taifa.
- Hali ya Amani na Utulivu idumishwe, na Baraza limeihimiza Serikali kuchukua hatua kali za haraka kwa wanaofanya vitendo vya uvunjifu wa sheria.
- Baraza Kuu limeitaka Serikali kurekebisha syllabus na kuongeza somo la ujasiriamali.
- Limeitaka serikali kuboresha na kuvisimamia kwa ukamilifu vyuo vya mafunzo stadi, pamoja na SIDO
- Pia Baraza Kuu limeitaka Serikali kutowasumbua vijana wasio na ajira rasmi kama Machinga, Bodaboda n.k na kuacha kutumia matumizi ya nguvu ya dola yasiyokuwa ya lazima katika kutatua matatizo yanayotokea kati ya Halmashauri za Miji na Vijana hawa.
- Baraza Kuu limehimiza Jumuiya kuendeleza jitihada za kujitegemea na kuinua mapato ya jumuiya.
- Lakini pia, Baraza Kuu limeitaka Mikoa kujiimarisha kinidhamu, na kuwataka wajumbe kufuata kanuni na taratibu za umoja wa Vijana ili kuepusha mkanganyingo na utovu wa nidhamu.
Pamoja na Maazimio hayo, Baraza Kuu pia limetoa TAMKO la kulaani mauaji yaliyojitokeza katika vurugu za kidini katika eneo la Busesere, wilayani geita lakini pia Baraza limelaani vikali mauaji ya Padri Evarist Mushi wa Parokia ya Minara Miwili-Mtoni Kijichi yaliyotokea jana asubuhi Zanzibar. Wameitaka Serikali Kuwachukulia hatua kali wale wote waliohusika lakini pia imetoa pole kwa familia, wakatoliki na watanzania wote kwa ujumla kutokana na msiba huo.