.
- Asema wananchi wanakerwa na fujo zao bungeni.
- Adai zitapunguza idadi ya wabunge wao bungeni.
- Zitashusha hadhi yao kwa umma.
- Asema walitumwa kutetea wananchi, si kufanya fujo.
Juliana Shonza akihutubia wakazi wa Temeke juu ya maamuzi yake thabiti ya kujiunga na CCM |
Mtela Mwampamba akiwaeleza wananchi wa Temeke mapungufu makubwa ya kidemokrasia yaliyopo kwenye vyama vya upinzani na hivyo kumfanya yeye binafsi kuchukua uamuzi wa kujiunga na CCM. |
Saumu Kisena akionyesha kitambulisho chake , Saumu amejiunga rasmi CCM baada ya kugundua chama alichokuwepo kinahubiri haki nje wakati ndani hamna haki kabisa. |
Katibu wa NEC ,Itikadi na Uenezi, akihutubia wananchi wa Wilaya ya Temeke na kuwahakikishia kuwa CCM itaisimamia serikali itekeleze ilani yake ya Uchaguzi kwa asilimia 100. |
Mkuu wa Wilaya ya Temeke ,Ndugu Sophia Mjema akiwapungia wananchi wa Temeke wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Pile ,Temeke ,Mwisho. |
Wananchi na Wapenzi wa CCM kutoka kata ya Kilakala,Yombo kama walivyojitambulisha ,walisema Nape ameongea mambo mengi ya msingi na kumtakia heri aendelee kufanya kazi nzuri. |
Wasanii wa kikundi cha TMK wakitoa burudani kwenye uwanja wa nyumbani wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Pile, Temeke,tarehe 16/2/2013. |
Baadhi ya wananchi wakionekana kuelewa vizuri maneno ya viongozi wao. |
Kikundi cha Hamasa cha CCM,Temeke kikihamasisha kwa aina yake wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Pile,Temeke. |