Google PlusRSS FeedEmail

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM BARA AWASILI KIGOMA LEO.

Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Ndugu philip Mangula akiteremka kutoka kwenye ndege ya shirika la ndege la Tanzania (Air Tanzania) ,kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma leo asubuhi tarehe 1/2/2013.
Makamu Mwenyekiti CCM Bara Philip Mangula  akipokelewa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Moses Nnauye mara baada ya kuwasili Kigoma asubuhi ya leo kwa ndege ya shirika la ndege la Tanzania (Air Tanzania)


Vijana Chipukizi wa CCM wakiimba kwa furaha wakati wa mapokezi ya Makamu Mwenyekiti  wa CCM- Bara,Ndugu Philip Mangula  kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma.



Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara,Ndugu Philip Mangula akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM mkoani Kigoma mara tu alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kigoma, uwanja ambao umefanyiwa maboresh makubwa ikiwa na kuongezwa sehemu ya kurushia ndege.

Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara ,Ndugu Philip Mangulaakitoa salaam za shukrani kwa mapokezi mazuri pia alitoa pongezi kwa maboresho ya uwanja wa ndege ambao alisema ni mzuri kulinganisha na miaka ya nyuma na amekiri kumekuwa na mabadiliko makubwa ya kimaendeleo katika mji wa Kigoma. Makamu Mwenyekiti amewasili rasmi kwa ajili ya sherehe za miaka 36 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi ambazo kitaifa mwaka huu zitafanyika tarehe 3/2/2013 mkoani kigoma kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika.

This entry was posted in

Leave a Reply