NA BASHIR NKOROMO
Familia ya Joseph Nyerere, imejitokeza na kusema haimtambui mtuhumiwa wa kesi ya mauaji, anayejitambulisha kwa jina la Makongoro Joseph Nyerere.
Taarifa iliyotolewa na Nuru Nyerere-Inyangete, kwa niaba ya familia hiyo jana, ilisema hadi kifo cha baba yao, Joseph Kizurira Nyerere, mwaka 1994 haina taarifa zozote za kuwa na ndugu yao anayeitwa Makongoro Joseph Nyerere.
“Hadi baba anafariki dunia hatukuambiwa tuna ndugu anayeitwa Makongoro Joseph Kizurira Nyerere …watoto wote wa Mzee Joseph tunafahamiana, lakini kwa huyu ndiyo kwanza tunaambiwa kuwa ni ndugu yetu. Tunauhakikishia umma kwamba hadi kifo cha baba yetu hatukuambiwa juu ya kuwapo kwa ndugu mwenye jina hilo; hii ina maana kwamba hatumtambui,” alisema Nuru.
Naye mtoto mwingine wa Joseph, Matare, alisema, “Tangu kutangazwa kwa habari hizi tunapata simu nyingi za pole. Tunashangaa kwa sababu huyu mtu hatukuwahi kuambiwa kuwa ni ndugu yetu, na wala yeye mwenyewe hakuwahi kuja kwetu kujitambulisha kama ni mmoja wa watoto wa Mzee Joseph.”
Matare aliongeza, “Tumesoma kwa mshituko kwenye magazeti ya Februari 14, 2013 na katika mitandao ya kijamii, kuwa kuna mtu anayejiita Makongoro Joseph Nyerere. Huyu huyu hatumtambui kwa uhusiano, taarifa wala sura. Watoto wote wa marehemu Joseph Nyerere wanafahamika, hakuna mtoto wa marehemu mwenye jina hilo.”
Juzi, Makongoro ambaye ni mfanyabiashara, mkazi wa Dar es Salaam, alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini humo akikabiliwa na mashitaka ya mauaji ya mfanyabiashara mwenzake, Onesphory Kitoli. Mtuhumiwa huyo anatarajiwa kuunganishwa katika kesi hiyo na mtuhumiwa mwingine mfanyabiashara maarufu, Marijani Abubakari marufu kama Papaa Msofe (50). Kesi hiyo itatajwa Februari 20, mwaka huu.
Wakili wa Serikali, Charles Anindo, alimsomea Makongoro mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi, Agnes Mchome, na kudai kuwa Novemba 6, 2011 huko Magomeni Mapipa, Makongoro alimuua kwa makusudi Kitoli kinyume na kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002.
Anindo alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na aliomba Mahakama iahirishe kesi hiyo hadi Februari 20, mwaka huu, ambako Makongoro ataunganishwa na Papaa Msofe kwenye mashitaka hayo.
Mtuhumkiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
-
▼
2013
(633)
-
▼
February
(55)
- SADIFA AONGOZA MASHAMBULIZI YA UVCCM MKOANI MOROGORO
- TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA WADAU WA PSPF KUFANYIKA...
- WAZIRI MKUU AZINDUA MPANGO MKAKATI WA GS1 TANZANIA
- OFISA TABIBU WA BUNDA MATATANI KWA KUMTOA MIMBA MH...
- MeTL GROUP YAPOKEA TUZO
- SERIKALI YATAKIWA KUTILIA MKAZO MCHEZO WA KUOGELEA
- NAIBU WAZIRI WA FEDHA AKAGUA VITEGAUCHUMI VYA VYA ...
- WADAU WA PSPF WAONESHWA NYUMBA ZA MKOPO ZILIZOPO B...
- SHINA LA PAMBA ROAD LAFANYA UCHAGUZI.
- MJUMBE WA NEC, MAMA SALMA KIKWETE AMALIZA ZIARA LI...
- RAIS WA KENYA AZINDUA BARABARA YA MWAI KIBAKI JIJI...
- KINANA AKUTANA NA MABALOZI LEO
- MJUMBE WA NEC, MAMA SALMA KIKWETE AMALIZA ZIARA LI...
- NAPE ASEMA NA WANACCM WA TAWI LA OFISI NDOGO DAR !!
- ZAIARA YA MAMA JK LINDI YAZIDI KUNOGA, LEO YUPO KA...
- MAMA SALMA KIKWETE LEO YUPO KATA YA MBANJE
- KIKAO CHA BARAZA KUU LA UVCCM TAIFA CHAMALIZIKA, W...
- NAPE AITEKA GOBA LEO
- SEMINA YA HALI YA ELIMU NA AJIRA KWA WAJUMBE WA BA...
- MATUKIO-KIKAO CHA BARAZA KUU LA UVCCM TAIFA.
- ZIARA YA MAMA SALMA KIKWETE LINDI YAZOA WANACHAMA...
- NAPE : CHADEMA ACHENI KULIALIA.
- NAPE; BUNGE KURUSHWA LIVE KUTAIMALIZA CHADEMA
- UN: MAZUNGUMZO DAWA YA MIGOGORO YA KIDINI
- KIKAO CHA BARAZA KUU LA UVCCM TAIFA, DODOMA
- ZIARA YA MAMA SALMA LINDI, AFANYA MIKUTANO KIBAO Y...
- FAMILIA YAMKANA ANAYEJIITA MAKONGORO NYERERE
- ZIARA YA MAMA SALMA KIKWETE LINDI MJINI LEO
- MAMA SALMA KIKWETE AMFARIJI WAZIRI HAWA GHASIA KWA...
- TAMKO LA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM KUHUSU MA...
- VICHWA VYA HABARI KAMA HIKI KWENYE MAGAZETI VINASA...
- JULIANA SHONZA NA MTELA MWAMPAMBA WAJIUNGA NA CCM ...
- ZOEZI LA UPIGAJI KURA LILIVYOENDESHWA PICHANI
- TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
- BIASHARA YA MAGAZETI KWENYE MKUTANO WA NEC YA CCM ...
- SEMINA YA MIKAKATI YA KUONDOA TATIZO LA AJIRA NCHINI
- RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA SEMINA YA WAJUMBE WA N...
- RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AWASILI DODOMA JIONI HII
- TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
- MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ALIPOKUTANA NA SENETA STI...
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL KATIKA PICHA ZA MATUKIO ...
- RAIS KIKWETE ASHIRIKI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU Y...
- UKEKETAJI NI UKATILI:WIZARA
- MAADHISHO YA MIAKA 36 YA CCM MKOANI LINDI
- POLISI ANAPOSHIRIKI KUVUNJA SHERIA ZA USALAMA BARA...
- WAJAWAZITO WILAYANI KILWA WAPATA VITANDA VYA UZAZI.
- RAIS KIKWETE AKAGUA UJENZI DARAJA LA KIKWETE,KIGOMA
- SHEREHE ZA MIAKA 36 YA CCM ZAFANA KIGOMA, MAELFU W...
- MWENYEKITI WA CCM RAIS KIKWETE AONGOZA MATEMBEZI Y...
- RAIS KIKWETE APATA MAPOKEZI MAKUBWA KIGOMA
- KATIBU MKUU WA CHAMA CHA PPRD AWASILI KIGOMA LEO.
- KINANA AFUNGA KAZI KIBONDO KWA MKUTANO MKUBWA WA H...
- MAKAMU MWENYEKITI WA CCM BARA AWASILI KIGOMA LEO.
- MATUKIO MBALI MBALI YA ZIARA YA DK.MIGIRO ,KATIKA ...
- KINANA ASHIRIKI KAZI ZA JAMII KIBONDO
-
▼
February
(55)
LOVE LINKS
Powered by Blogger.