Google PlusRSS FeedEmail

SHEREHE ZA MIAKA 36 YA CCM ZAFANA KIGOMA, MAELFU WAJITOKEZA

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili kwenye Uwanja wa Lake Tangayika kuongoza wananchi katika kilele cha sherehe za miaka 36 ya CCM, leo,
Wananchi wakichangamkia kumsalimia Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alipowasili Uwanja wa Lake Tanganyika leo kwenye sherehe hizo
Wananachi wakimshangilia Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akipoingia uwanjani kwenye sherehe hizo
Rais Kikwete akitazama ngoma ya Warundi waliokuwa wakitumbuiza wakati wa sherehe hizo. Pamoja naye ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kianana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba.
Mtoto ambaye ni msanii kutoka kundi hilo la Warundi akimkubatia Nape, alipokuwa akishuhudia ngoma yao
Vijana wa CCM wakipita kwa Ukamavu mbele ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete wakati wa gwaride maalum la vijana hao la maadhimisho ya sherehe hizo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa amesimama kupokea heshima wakati gwaride maalum la Vijana wa CCM, wakati wa sherehe hizo. Wengine kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Phili Mangula, na kulia ni Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Amani Kaborou
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihamasisha wananchi kuchangamsha sherehe hizo
 Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza kwenye sherehe hizo, huku Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimfuatilia kwa makini
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi kwenye mkutano huo. Kushoto ni Nape
 Wananchi wakiwa wamefurika Uwanjani wakati wa sherehe hizo, kiasi cha baadhi kualazimika kushika viatu mkononi kama huyu anayeshangilia
Diamond akitumbuiza kwenye sherehe hizo.
Msongamano mkubwa uwanjani kutokana na maelfu waliohudhuria sherehe hizo
Waalikwa kutoka Chama tawala cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakiwa na bendera yao kwenye sherehe hizo
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akihutubia maelfu ya wananchi kwenye sherehe hizo
Kikwete akisisitiza jambo wakati akihutubia kwenye sherehe hizo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akitazama ndizi zilizokuwa zikionyeshwa kwenye banda la Wakulima wa Kasulu mkoani Kigoma nye ya Uwanja wa Lake Tanganyika
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akitazama moja ya moja zilizovuta kumbukumbu zake, kwenye banda ya  Uhuru Publications Limited, wachapishaji wa magazeti ya Chama ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, kwenye banda la kampuni hiyo, nje ya Uwanja wa Lake Tanganyika. Pamoja naye ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Kulia ni Mhariri Mtendaji wa kampuni hiyo, Josiah Mufungo
 Hali iliyokuwa ikionekana nye ya Uwanja wa Lake Tanganyika wakati wa sherehe hizo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

This entry was posted in

Leave a Reply