Google PlusRSS FeedEmail

ZIARA YA MAMA SALMA KIKWETE LINDI MJINI LEO

 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wilaya ya Lindi mjini, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akimsalimia mwananchi baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara aliohutubia katika kijiji cha Nanyanje, Kata ya Chikonje wilayani humo leo, akiwa katika ziara ya siku saba kukagua na kuimarisha uhai wa Chama na Utekelezaji wa ilani.
 Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji hicho cha  Nanyanje, wilaya ya Chikonje, wilaya ya Lindi mjini leo
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Kata ya Chikonje, wakimsikiliza Mama Salma Kikwete alipozungumza nao katika kikao cha ndani, kwenye Ofisi ya CCM ya Kata hiyo leo.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Mama Salma Kikwete akipokea kadi ya CUF kutoka kwa aliyekuwa mwanachama wa chama hicho, Salma Saidi (kushoto) baada ya kutangaza kuhamia CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha  Nanyanje, Kata ya Chikonje mkoani Lindi leo
  Wanachama wapya wa CCM waliokabidhiwa kadi zao wakiwemo kutoka vyama vya CUF na Chadema, wakila kiapo baada ya kukabidhiwa kadi zao na Mama Salma Kikwete leo
 Mama Salma Kikwete akishiriki kucheza ngoma ya zindiko ya wakazi wa Chikonje, iliyotumbuiza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika leo

 Wasanii wa kundi la ngoma ya zindiko ya Chikonje wakionyesha umahiri wao katika mkutano huo
 Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo wa kijiji cha Nanyanje kata ya Chikonje mkoani Lindi
 Wananchi wakiselebuka kwa nyimbo za CCM wakati wa mkutano huo
Ilikuwa aisye na mwana aelekee jiwe: mama akiwa na watoto wake kwenye mkutano huo. (picha zote na Bashir Nkoromo).

This entry was posted in

Leave a Reply