Picha ya pamoja ya wanachama na wajumbe wa mkutano wa Uchaguzi wa Viongozi wa Shina la Pamba Road uliofanyika leo katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam. |
Na Adam Mzee, Dar es salaam.
Shina la Chama cha Mapinduzi la Pamba road lenye maskani yake eneo la Posta, Jijini dar es salaam limefanya Uchaguzi wa muda kwa nafasi ya Mwenyekiti na Mjumbe, kupelekea Mwenyekiti wake wa zamani Ndugu Said Salum Masanga kujiuzulu nafasi hiyo kwa kuwa amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Vijana wa CCM Wilaya ya Kinondoni.
Ambapo kutokana na Katiba na Kanuni ya Uongozi za Chama cha Mapinduzi, kuwa Mwanacha hawezi kuwa na vyeo viwili vya kutumikia katika wakati mmoja, hivyo Ndugu Masanga alijiuzulu na kuacha wazi nafasi ya Mwenyekiti wa Shina Hilo.
Kwa nafasi ya Mwenyekiti wa Shina Hilo, walijitokeza watu watatu ambao walipitishwa na vikao vya ndani na hivyo kupitisha majina yao ili yaweze kupigiwa kura, ambao ni;
1) Khamis Nshimba
2) Ramadhani Makula
3) Dr Richard Manunu
Ambapo Ndugu Ramadhani Makula aliibuka mshindi kwa nafasi hiyo na kutangazwa kama kiongozi halali na Mwenyekiti wa Shina hilo lililopo katikati ya Jiji.
Kwa nafasi ya Ujumbe walijitokeza watu wawili ambao ni;
1) Allen Malewah
2) Sophia Mbwile.
Ambapo Ndugu Sophia Mbwile aliibuka Mshindi.
Mkutano huo wa Uchaguzi ulifanyika katika ukumbi wa Karimjee ambapo ulihudhuriwa na waalikwa nawageni mbalimbali, akiwemo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa akiwakilisha wilaya ya Bagamoyo Ndugu Ridhwani Kikwete na Paul Christian Makonda (Aliyegombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti UVCCM Taifa), Mwenyekiti wa Kikao hicho kwa muda ndugu Augustino Matefu na wengineo.
Uchaguzi huo ambao ulikuwa wa haki na huru ulimalizika salama Jioni ya leo ambapo hakuna mgombea yeyote aliyejitokeza kupinga ama kulaumu kutotendewa haki.