Google PlusRSS FeedEmail

NAPE AITEKA GOBA LEO

Umati wa wananchi wa Goba ulikuja kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na CCM Mkoa wa Dar es salaam.

Mtela Mwambpamba akihutubia wananchi wa Goba sababu zilizomfanya ajiunge na chama cha CCM.

Juliana Shonza aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA,akihutubia wakazi wa Goba na kuwaambia  ndani ya Chadema hakuna haki wala usawa .

Mwenyekiti wa CCM ,Mkoa wa Dar es salaam akihutubia wananchi wa Goba katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo ,Feb 17, 2013.

Mwenyekiti wa  CCM Kata ya Goba,Theresia Chihota akiukaribisha ugeni kutoka CCM Mkoa wa Dar es salaam na CCM Taifa ambao walifika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Goba,Feb 17, 2013.

Sura za furaha zinazoashiria jimbo la Ubungo linarudi CCM

Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi ,Nape Nnauye amekabidhi pikipiki kwa vijana wa Goba kwa shughuli za ujasiriamali,pia amewapa wakina mama wenye kikundi cha Vikoba shilingi milioni moja na pia ameahidi kuongeza pikipiki na jezi za timu ya mpira.

Mkutano wa hadhara wa CCM, uliofanyika Goba umeongeza wananchama wapya 162, na wengine wanne kutoka chama cha upinzani,pichani mmoja wa aliyekuwa mwanachama wa Chadema akirudisha kadi yake na kujiunga na CCM.

Profesa Jumanne Maghembe akihutubia wakazi wa Goba na kuto majibu ya kuridhisha kuhusu mikakati na mipango ya kuleta maji Goba. 

This entry was posted in

Leave a Reply