Google PlusRSS FeedEmail

RAIS KIKWETE APATA MAPOKEZI MAKUBWA KIGOMA

Kikundi cha Ngoma cha Wakinamama wa Kigoma kikitumbuiza  wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi,Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
Ndege ya Rais  Kikwete ikiwasili Kigoma  leo tayari kwa sherehe za miaka 36 ya CCM zitakazo fanyika kesho Kigoma kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika.


Rais Kikwete akiteremka kwenye ndege leo  katika uwanja  wa ndege wa Kigoma tayari kwa sherehe za miaka 36 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi.
Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na mjumbe wa  NEC Wilaya ya Kigoma  mjini, Kilumbe Ng'enda mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Kigoma leo tayari kwa sherehe za kuzaliwa kwa CCM.


Mwenyekiti wa CCM akisalimiana na wananchi wa Kigoma waliokuja kwa wingi kumpokea , Mwenyekiti yupo Kigoma kwa ajili ya sherehe za miaka 36 ya CCM.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ndio Mwenyekiti wa CCM,akiwa pamoja na Nape Nnauye Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi kwenye uwanja wa ndege Kigoma.

Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza mtangazaji wa Radio Uhuru ,Stephen Mhina ambaye alitaka  kujua pamoja na maendeleo yote yaliofanyika Kigoma, Mheshimiwa rais alimjibu kuwa "tunatimiza wajibu"

This entry was posted in

Leave a Reply