MAMA SALMA KIKWETE |
NA BASHIR NKOROMO, LINDI
ZIARA ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi, Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete mkoani hapa,imeendelea kuzaa matunda baada ya wanachama wapya 189 wakiwemo waaliokuwa wanachama wa CUF kujiunga na CCM.
Ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake hiyo ambayo ni mahsuisi kukagua na kuimarisha uhai wa chama na pia kuwashukuru Wana-Lindi kwa kumchagua kwa kura zote kuwa mjumbe wa NEC, Mama Salma alipokea wanachama hao katika mikutano ya hadhara iliyofanyika katika kata zaTandangongoro, Ng'apa na Rahaleo zilizopo katika wilaya ya Lindi mjini.
Katika kata ya Tandangongoro wanachama walijiunga 37 wakiwemo watano kutoka CUF,kata ya Ng'apa 93 WAKIWEMO 30 kutoka CUF na kata ya Rahaleo wanachama 59.
Akiwakabidhi kadi hizo baada ya kupokea waliotoka CUF Mama Salma aliwapongeza kwa uamuzi waliochukua wa kujiunga na CCM akisema hekima yao imewafanya kuingia CCM kwa kuwa wanatambua kuwa hakuna Chama kingine kinachoweza kuwaleta maendeleo.
" Hii ndo CCM ikiahidi inatekeleza kwa asilimia 100 kwa sababu inatambua matatizo ya wananchi na inadhamira ya dhati ya kuyatatua, endeleeni kukichangua Chama Cha Mapinduzi kwa sababu ndicho kitakachoendelea ndani ya vyama vingi, kwa kuwa kina sera makini zinazotekelezeka," alisema.
Baadhi ya wanachama waliotoka CUF walisema kwamba hawakushurutishwa na yeyote kujiunga na bali wamefanya hivyo kwA hiari yao baada ya kuona jinsi CCM inavyotekeleza Ilani yake ya uchaguzi na kueleza kwamba wana matumaini Chama hicho kitafanya mengi na kuahidi kurudisha jimbo la Lindi Mjini.
Wakishangiliwa na mamia ya wananchi katika mikutano hiyo baadhi yao walisema waliokuwa CUF kutokana na kurubuniwa na maneno ya ghiriba yaliyowapa matumaini kwamba huenda wanaweza kuwaletea maendeleo makubwa jambo wamegundua kwamba haiweszekani kwa sababu hawana sera za kusimamia ahadi zao.