Na Abdulaziz Video
AKINA mama wajawazito katika wilaya ya Kilwa mkoani Lindi,wameanza kuondokana na tatizo la kukosa vifaa wakati wa kujifungua,baada ya Halmashauri ya wilaya hiyo kununua vitanda kumi (10) vitakavyotumika kutolea huduma ya kujifungulia. Kununuliwa kwa vitanda hivyo ni utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete,alilolitoa hivi Mwishoni mwa Mwaka jana alipokuwa katika ziara ya kukagua shughuli za Maendeleo zinazotekelezwa katika Mkoa huo ambapo aliiagiza Halmashauri hiyo kununua kitanda baada ya kupokea kero hiyo katika Kata ya Mitole Wilayani Kilwa, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo,Addoh Mapunda, Akiongea na mtandao Ameeleza kuwa kununuliwa kwa vitanda hivyo 10 ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais.
Kutokana na agizo la Rais,Halmashauri ya wilaya hiyo Imenunua vitanda zaidi ili kusaidia zahanati kumi kati ya 46 zilizopo ndani ya wilaya hiyo. Zahanati zilizonufaika na mpango huo ni,Mt Kimwaga,Nandembo,Kisangi, Kimbarambara,Kibata,Ngarambe,
Hivi karibuni Mkuu wa Wilaya ya Kilwa,Abdallah Hamisi Ulega alikabidhi Kitanda cha Zahanati ya Mitole ambapo wananchi walitoa kero hiyo kwa Rais Sambamba na kununuliwa kwa vitanda hivyo,Halmashauri hiyo pia imenunua seti (12) za kuzalishia ambapo kila seti moja imegharimu kiasi cha Sh,400,000/=
Decemba 04 mwaka jana, Rais Jakaya Kikwete, alipotembelea Shule ya Sekondari ya kata ya Mitole iliyopo wilayani Kilwa,katika risala yao wananchi walimuomba kuwasaidia kuwapatia kitanda kwa ajili ya kujifungulia akina mama wajawazito,ambapo naye aliuagiza uongozi wa Halmashauri hiyo kutekeleza hilo.
Moja ya vitanda ambavyo vimenunuliwa na halmashauri ya mji wa kilwa ili kusaidia akina mama wajawazito. |