Google PlusRSS FeedEmail
Na Abdulaziz Video

AKINA mama wajawazito katika wilaya ya Kilwa mkoani Lindi,wameanza kuondokana na tatizo la kukosa vifaa wakati wa kujifungua,baada ya Halmashauri ya wilaya hiyo kununua vitanda kumi (10) vitakavyotumika kutolea huduma ya kujifungulia. Kununuliwa kwa vitanda hivyo ni utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete,alilolitoa hivi Mwishoni mwa Mwaka jana alipokuwa katika ziara ya kukagua shughuli za Maendeleo zinazotekelezwa katika Mkoa huo ambapo aliiagiza Halmashauri hiyo kununua kitanda baada ya kupokea kero hiyo katika Kata ya Mitole Wilayani Kilwa, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo,Addoh Mapunda, Akiongea na mtandao Ameeleza   kuwa kununuliwa kwa vitanda hivyo 10 ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais.

Kutokana na agizo la Rais,Halmashauri ya wilaya hiyo Imenunua vitanda zaidi ili kusaidia zahanati kumi kati ya 46 zilizopo ndani ya wilaya hiyo. Zahanati zilizonufaika na mpango huo ni,Mt Kimwaga,Nandembo,Kisangi, Kimbarambara,Kibata,Ngarambe,Tingi na Kanadawale, Jimbo la Kilwa kaskazini, ambapo kwa Jimbo la Kilwa kusini ni,Rushungi,Pande na Mitole.

 Hivi karibuni Mkuu wa Wilaya ya Kilwa,Abdallah Hamisi Ulega alikabidhi Kitanda cha Zahanati ya Mitole ambapo wananchi walitoa kero hiyo kwa Rais Sambamba na kununuliwa kwa vitanda hivyo,Halmashauri hiyo pia imenunua seti (12) za kuzalishia ambapo kila seti moja imegharimu kiasi cha Sh,400,000/=

 Nae, Addoh Mapunda,Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo amesema kununuliwa kwa vitanda hivyo, sio tu ni utekelezaji wa agizo la Rais Kikwete, pia ni uendelezaji wa utekelezaji wake, kwani tayari Zahanati 36 kati ya hizo 46 zilikwisha nunuliwa vitanda vya aina hiyo na kufanya Zahanati zote kuondokana na tatizo hilo kwa sasa Ni kweli Zahanati za Kilwa na Jiografia ya kufika Hospital ya Wilaya au Mkoa ni Ngumu sana ila Jitihada za Idara ya Afya,Pamoja na Utawala yaani Ofisi yangu Tukishirikiana na Mkuu wa Wilaya kwa kutafuta Ufadhili Tumeanza kujidhatiti kusaidia Jamii ila Naomba Hata Madiwani Watupe Ushirikiano kwa kuwa wao kwa kushirikiana na watendaji na Wenyeviti wa Vijiji Watasaidia kushauri ili sisi Tujikite katika Uboreshaji wa Huduma kwa Karibu.Alimalizia Mapunda.

Decemba 04 mwaka jana, Rais Jakaya Kikwete, alipotembelea Shule ya Sekondari ya kata ya Mitole iliyopo wilayani Kilwa,katika risala yao wananchi walimuomba kuwasaidia kuwapatia kitanda kwa ajili ya kujifungulia akina mama wajawazito,ambapo naye aliuagiza uongozi wa Halmashauri hiyo kutekeleza hilo.


 Mkuu wa wilaya ya Kilwa Mheshimiwa Abdallah hamis Ulega akiwa pamoja na mkurugenzi na watendaji wengine wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa katika zoezi la kukabidhi vitanda na seti za kuzalishia kwa hospitali na zahanati zilizopo katika halmashauri hiyo.

Moja ya vitanda ambavyo vimenunuliwa na halmashauri ya mji wa kilwa ili kusaidia akina mama wajawazito.

WAJAWAZITO WILAYANI KILWA WAPATA VITANDA VYA UZAZI.

Na Abdulaziz Video AKINA mama wajawazito katika wilaya ya Kilwa mkoani Lindi,wameanza  kuondokana na tatizo la kukosa vifaa wakati wa kujifu... [Read More]

 Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wananchi wa Uvinza mkoani Kigoma wakati akiwa njiani kwenda kukagua ujenzi wa daraja la Kikwete kwenye mto Maragarasi mkoani humo leo mchana
 Wananchi na wafanyakazi wa kampuni ya Hanil Engeneering ya Korea wakimsubiri Rais Kikwete kwenye ifisi ya mradi wa ujenzi wa barabara hiyo.
 Rais Jakaya Kikwete akimsalimia Waziri wa Kilimo na Chakula Injinia Christopher Chiza baada ya kuwasili kwenye Ofisi za mradi wa ujenzi wa Daraja la Kikwete kwenye mto Maragarasi mkoani Kigoma. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Danih Makanga
 Rais Kikwete akiwasalimia wafanyakazi wa kampuni ya Hanil ya Korea. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Khadija Nyembo na wapili ni DC wa Kasulu Danih Makanga.
Meneja Mradi wa Ujenzi dsaraja la Kikwete katika mto Maragarasi mkoani Kigoma, Crispinas Ako (aliyevyoosha mkono) akimpatia maelezo Rais Jakaya Kikwete kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi huo alipotembelea leo
 Daraja linalotumiwa na treni kwenye mto Maragarasi ambako pembeni yake ndiko linalojengwa litakalotumiwa na magari kutoka Tabora kwenda Kigoma
 Rais Jakaya Kikwete (kushoto) akikagua ujenzi wa darala la Kikwete kwenye mto Maragarasi mkoani Kigoma leo.
 Msafara wa Rais Kikwete ukipita kwenye darala la Kikwete ambalo ujenzi wake unaedelea kwenye mto Maragarasi mkoani Kigoma
Rais Kikwete akizungumza na wananchi wa Maragalasi baada ya kukagua ujenzi wa daraja la Kikwete katika mto Maragalasi leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

RAIS KIKWETE AKAGUA UJENZI DARAJA LA KIKWETE,KIGOMA

 Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wananchi wa Uvinza mkoani Kigoma wakati akiwa njiani kwenda kukagua ujenzi wa daraja la Kikwete kwenye m... [Read More]

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili kwenye Uwanja wa Lake Tangayika kuongoza wananchi katika kilele cha sherehe za miaka 36 ya CCM, leo,
Wananchi wakichangamkia kumsalimia Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alipowasili Uwanja wa Lake Tanganyika leo kwenye sherehe hizo
Wananachi wakimshangilia Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akipoingia uwanjani kwenye sherehe hizo
Rais Kikwete akitazama ngoma ya Warundi waliokuwa wakitumbuiza wakati wa sherehe hizo. Pamoja naye ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kianana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba.
Mtoto ambaye ni msanii kutoka kundi hilo la Warundi akimkubatia Nape, alipokuwa akishuhudia ngoma yao
Vijana wa CCM wakipita kwa Ukamavu mbele ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete wakati wa gwaride maalum la vijana hao la maadhimisho ya sherehe hizo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa amesimama kupokea heshima wakati gwaride maalum la Vijana wa CCM, wakati wa sherehe hizo. Wengine kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Phili Mangula, na kulia ni Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Amani Kaborou
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihamasisha wananchi kuchangamsha sherehe hizo
 Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza kwenye sherehe hizo, huku Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimfuatilia kwa makini
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi kwenye mkutano huo. Kushoto ni Nape
 Wananchi wakiwa wamefurika Uwanjani wakati wa sherehe hizo, kiasi cha baadhi kualazimika kushika viatu mkononi kama huyu anayeshangilia
Diamond akitumbuiza kwenye sherehe hizo.
Msongamano mkubwa uwanjani kutokana na maelfu waliohudhuria sherehe hizo
Waalikwa kutoka Chama tawala cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakiwa na bendera yao kwenye sherehe hizo
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akihutubia maelfu ya wananchi kwenye sherehe hizo
Kikwete akisisitiza jambo wakati akihutubia kwenye sherehe hizo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akitazama ndizi zilizokuwa zikionyeshwa kwenye banda la Wakulima wa Kasulu mkoani Kigoma nye ya Uwanja wa Lake Tanganyika
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akitazama moja ya moja zilizovuta kumbukumbu zake, kwenye banda ya  Uhuru Publications Limited, wachapishaji wa magazeti ya Chama ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, kwenye banda la kampuni hiyo, nje ya Uwanja wa Lake Tanganyika. Pamoja naye ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Kulia ni Mhariri Mtendaji wa kampuni hiyo, Josiah Mufungo
 Hali iliyokuwa ikionekana nye ya Uwanja wa Lake Tanganyika wakati wa sherehe hizo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

SHEREHE ZA MIAKA 36 YA CCM ZAFANA KIGOMA, MAELFU WAJITOKEZA

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili kwenye Uwanja wa Lake Tangayika kuongoza wananchi katika kilele cha sherehe za miaka 36 ya ... [Read More]

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akiongoza matembezi ya maadhimisho ya miaka 36 ya CCM, leo asubuhi kutoka eneo la Mnarani hadi ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma leo. Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Amani Kaborou, Mama Salma Kikwete, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kulia)
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiongoza matembezi ya mshikamano ya Miaka 36 ya CCM, mjini Kigoma leo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiongoza matembezi ya Mshikamano ya Maadhimisho ya Miaka 36 ya CCM mjini Kigoma leo
Matembezi hayo yakipita eneo la Burega, Barabara ya Kigoma-Ujiji
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akiwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Sadifa Abdalla na Mkuu wa wilaya ya Kigoma Jumanne Maneo
Wananchi wakishangilia wakati matembezi yakipita barabara ya Ujiji Kigoma kwenda Ofisi ya CCM ya mkoa wa Kigoma leo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimsalimia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana baada ya kuwasili eneo la Mnarani mjini Kigoma tayari kwa matembezi hayo. Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula na wengine ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwapungia mkono wananchi msafara wa matembezi hayo ulipokaribika kufika Ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma
Rais Kikwete akiwa na Nape na Kinana baada ya msafara wa matembezi hayo kuwasili
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikweye akiwa na muaasisi mmoja wa CCM ( ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja) baada ya matembezi kufika Ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma
 
 Mama Salma Kikwete akisalimia baada ya msafara wamatembezi hayo kufika Ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma
Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete na msafara wake wakiwa wameketi meza kuu Ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma baada ya matembezi hayo.
"NDUGU WANANCHI, NAWAPONGEZA KWA KUSHIRIKI KWA WINGI KWENYE MATEMBEZI HAYA. HAPA SISEMI MENGI TUKUTANE MCHANA PALE UWANJA WA LAKE TANGANYIKA" Akasema Rais Kikwete wakati akizungumza na wananchi baada ya matembezi hayo. (PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO@Daily Nkoromo Blog)

MWENYEKITI WA CCM RAIS KIKWETE AONGOZA MATEMBEZI YA MSHIKAMANO YA MIAKA 36 YA CCM MJINI KIGOMA LEO

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akiongoza matembezi ya maadhimisho ya miaka 36 ya CCM, leo asubuhi kutoka eneo la Mnarani hadi ofisi y... [Read More]

RAIS KIKWETE APATA MAPOKEZI MAKUBWA KIGOMA

Kikundi cha Ngoma cha Wakinamama wa Kigoma kikitumbuiza  wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi,Dk.Jakaya Mrisho Kikwete. N... [Read More]