Google PlusRSS FeedEmail
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Maombi, Kata ya Mbalizi, Mbeya Vijijini, jana, Des 3, 2013, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua mkoani Mbeya.
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mbeya mjini, Ephraim Mwaitenda akiwatambulisha viongozi wake kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, katika mapokezi kuingia mbeya mjini
 Vijana wakiwa na mabango wakati wa mapokezi ya Kinana kutoka Mbeya Vijijini kuingia Mbeya mjini leo asubuhi
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA Richard Festo, alipowasili leo kwenye stesheni ya Reli hiyo mjini Mbeya, kuzungumza na wafanyakazi wa shirika hilo la reli, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua mkoani Mbeya.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA), leo Des 4, 2013, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua mkoani Mbeya. Wengine kutoka kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Mbunge Mteule, Dk. Asha-Rose Migiro na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na Mbunge wa Mbozi Mashariki Godfrey Zambi.
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Mbunge Mteule, Dk. Asha-Rose Migiro akiwasalimia wafanyakazi wa TARAZA kwenye mkutano huo na Kinana
 Mwenyekiti wa Wafanyakazi wa TAZARA Ally Mkami akisoma risala ya wafanyakazi
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwasalimia wafanayakazi wa TAZARA
 Wafanyakazi wa TAZARA wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipozungumza nao leo mjini Mbeya
 Katibu wa NEC, Itikasi na Uenezi, Nape Nnauye akiwa ameketi kwenye mkeka na wananchi wengine, wakati wa kikao cha shina kilichofanyika  nyumbani kwa mjumbe wa shina namba 14, mjini Mbeya leo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpa kadi mmoja wa wanachama wapya Elizabeth Mwakalebela, wakati wa kikao kilichofanyika nyumbanbi kwa mjumbe wa shina namba 14, na kuhudhuriwa na Kinana, mjini Mbeya leo
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Mbunge mteule, Dk. Asha-Rose Migiro (kushoto) akiwa ameketi kweneye mkeka  na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mbeya Dk. Mary Mwanjelwa, katika kikao kilichofanyika nyumbani kwa mjumbe wa shina namba 14, Mbeya Mjini.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza kwenye kikao kilichofanbyika nyumbani kwa mjumbe wa shina namba 14, Mbeya mjini leo.

KINANA AMALIZA ZIARA MBEYA VIJIJINI, ATINGA MBEYA MJINI LEO ASUBUHI, AZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI WA TAZARA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Maombi, Kata ya Mbalizi, Mbe... [Read More]

Dk. Asha-Rose Migiro
DAR ES SALAAM, Tanzania
Rais, Dk. Jakaya Kikwete amemteua Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Maifa (UN) Mstaafu, Dk. Asha-Rose Migiro kuwa Mbunge.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jijini Dar es Salaam, imesema, Uteuzi huo ambao umetangazwa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, ulianza tangu jana, Dese,mba 2, 2013.


Dk. Asha-Rose Migiro kwa sasa ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, anayesimamia Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI).


Akizungumzia uteuzi huo, mjini Mbalizi jioni hii,  akiwa Mbalizi mkoani Mbeya, Dk. Asha-Rose amemshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa uteuzi, akisema  ameupokea kwa furaha, na kueleza kuwa kitendo hicho kinadhihirisha jinsi Rais Kikwete alivyo na imani naye pamoja na imani kwa Wanawake wa Tanzania
PONGEZI ...
 Kufuatia uteuzi huo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpongeza Dk.Asha-Rose Migiro leo jioni, mjini Mbalizi mkoani Mbeya ambako wapo katika ziara ya kukagua utekeleza wa ilani ya CCM, na kusikiliza kero za wananchi kwa lengo la kuzipatia ufumbuzi
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimpongeza kwa uteuzi huo wa Rais Kikwete
 Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akimpongeza Dk. Asha-Rose Migiro kwa uteuzi huo wa Rais
.Dk. Asha Rose Migiro akizungumza na waandishi wa habari waliomfuata kutaka kujua ameupokeaje uteuzi huo wa Rais Kikwete. Nape, Kandoro na Dk. Asha-Rose mwenyewe wapo Mbalizi, katika ziara ya Kinana kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua. Picha kwa hisani ya Kamanda wa Matukio Blog

RAIS KIKWETE AMTEUA DK. ASHA-ROSE MIGIRO KUWA MBUNGE, KINANA, NAPE NA KANDORO WAMPONGEZA WAKIWA MBEYA

Dk. Asha-Rose Migiro DAR ES SALAAM, Tanzania Rais, Dk. Jakaya Kikwete amemteua Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Maifa (UN) Mstaafu, Dk. Asha-Ro... [Read More]

 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi zahanati ya Shamwengo,Kata ya Inyala, Mbeya Vijijinikiwa ni shughuli yake ya kwanza kufanya baada ya kuanza ziara yake mchana huu katika wilaya ya Mbeya Vijijini. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Dk. Norman Sigala
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose  Migiro akishiriki ujenzi  zahanati ya Shamwengo Kata ya Inyala,Mbeya Vijijini
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akikagua ujenzi wa  mradi wa maji Kata ya Iwindi Mbeya Vijijini
 Kinana (aliyeshika tangi kushoto) akichungulia kina cha tanki, wakati akikagua ujenzi wa mradi wa maji kata ya Iwindi, Mbeya Vijijini
 Kinana akikatiza mitaa wakati akienda kwa mjumbe wa shina namba moja, Mtaa wa Nsalala, Barabara ya Tunduma. KUshoto ni Mkuu wa wilaya ya Mbeya Vijijini Dk. Norman Sigala
 Mjunmbe wa Shina namba moja, Lidya Mwangoka akifungua kikao cha shina lake, kilichohudhuriwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (watatu kusho), Kushoto ni Dk. Asha-Rose
Kinana akila mhindi nyumbani kwa balozi wa shina namba moja, Lidya Mwangoka, Mbeya Vijijini. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mbeya (V) Ipyana Seme
 Kinana akizindua shina la wakereketwa vijana wa CCM, Mshikamano Nsalala, Mbalizi, Mbeya Vijijini
 Wananchi mjini Mbarali Mbeya Vijijini wakiwa wamejipanga barabarani kushuhudia msafara wa Kinana
 Kinana akiongoza msafara wake katika barabara ya Mbalizi, Mbeya kwenda ukumbini kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM wiyala ya Mbeya Vijijini. Baadhi ya viongozi alio nao ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk Asha-Rose Migiro na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Mbeya Vijijini wakiwa ukumbini mjini Mbalizi tayari kuzungumza na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana

KINANA AWASILI MBEYA VIJIJINI MCHANA HUU

 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi zahanati ya Shamwengo,Kata ya Inyala, Mbeya Vijijinikiwa ni shughuli yake ya kwanza... [Read More]

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa shue ya Msingi Rujewa, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua, katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, Des 2, 2013.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia maelfu ya watu katika Uwanja wa shue la Msingi Rujewa, wilayani Mbarali katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua, katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, Des 2, 2013.
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akihutubia maelfu ya watu katika Uwanja wa shue la Msingi Rujewa, wilayani Mbarali katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua, katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, Des 2, 2013.
Maelfu ya wananchi wakiishangilia CCM, katika mkutano wa hadhara  uliofanyika Uwanja wa shuela Msingi Rujewa, wilayani Mbarali katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kukagua
utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua, katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, Des 2, 2013. 
 Kinana akitazama ngoma ya jamii ya wafugaji wa Kimasai kwenye mkutano wa hadhara, Rujewa,wilayani Mbarali, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua, katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, Des 2, 2013.
 Vijana wa Kimasai wakitoa burudani katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika Des 2, 2013,katika Kata ya Rujewa, wilatani Mbarali Mbeya
 Mabinti wa Kimasai wakishangilia katika mkutano wa hadhara wa CCM, uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kwenye uwanja wa shule ya msingi Rujewa wilayani Mbararli mkoani
Mbeya.
 Kinana akiwaaga wananchi baada ya kuwahutubia katika Uwanja wa shulke ya msingi  Rujewa, wilayani Mbarali, Mbeya Des 2, 2013.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akikagua eneo la mto unaosambaza maji kwa ajili ya mradi wa kilimo cha umwagiliaji wa Mwendamtifu, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua, katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, Des 2, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye. Mradi huo umeelezwa kuwa na mgogoromkubwa wa ardhi kati ya wananchi na mwekezaji mmoja katika eneo hilo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (watatu kushoto) akiwasili kwenye mkutanowa hadhara aliohutubia, kwenye Uwanja wa shule ya msingi Rujenwa, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua, katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, Des 2, 2013. Wengine kutoka kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Katibu wa CCM mkoawa Mbaya Maganga Sengerema, Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abas Kandoro na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua tawila CCM Ihanga, kata ya Rujewa, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua, katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, Des 2, 2013. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Godfrey Zambi na Watatu ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Rujewa, Widen Ndamu.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na msafara wake wakipokewa kwa shangwe na wananchi baada ya kuwasili katika Kata ya Rujewa, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua, katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, Des 2, 2013. Imetayarishwa na theNkoromo Blog.

KINANA AITEKA MBARALI, RUJEWA YARINDIMA, MAELFU YA WANANCHI WAJITOKEZA MKUTANO WA HADHARA

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa shue ya Msingi Rujewa, akiwa katika ziara ya kukagua... [Read More]

 KATIBU Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana akishiriki na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kati) na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha_rose Migiro, katika ujenzi soko la Kata ya Mwambani, Makongolosi, Chunya, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadili nao njia ya kuzitatua, mkoani Mbeya
 Nape na Dk Asha -Asha-Rose wakishuka baada ya kushiriki ujenzi soko la Kata ya Mwambani, Makongolosi, Chunya
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kulia) akikagua bweni la wasichana, shule ya sekondari Maweni, Kata ya Mwambani, Chunya, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadili nao njia ya kuzitatua, mkoani MbeyaDes Mosi, 2013. Wapili kushoto ni Mkuu wa shule hiyo Elly Mnyalape.
 Dk Asha-Rose  akiwa na wnafunzi wa kike shule ya sekondari Maweni, , Mwambani, Chunya
 Kinana akifunga skrubu wakati akiweka mlango kwenye nyumba ya walimu na watumishi wa hospitali, Saza, Chunya. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, wakishiriki ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya sekondari Kapalala, wilayani Chunya.
 HUMU YAMO MAJI KWELI? Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisikiliza kama tanki lina maji alipozindua mradi wa maji safi na salama katika Kijiji cha wafugaji cha Mteka, wilayani Chunya
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Gegwa Luhende baada ya kuzindua mradi wa maji safi na salama katika kijiji cha wafugaji wa Kisukuma cha Mteka, Chunya
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakilachakula cha asili ya jamii ya wafugaji wa Kisukuma, katika msitu wa kijiji cha wafugaji hao cha Mteka, Chunya
 Kinana akikagua lambo la kunyweshea mifugo katika kijiji cha wafugaji cha Mteka, Chunya
MTUMBIWI HUU UTATUMIA KUCHOTEA WANACHAMA: Katibu Mkuu wa CCM Abdul;rahman  Kinana akiwa na zawadiza mtumbwi aliopewa na wazee katika kijiji cha Udinde, Chunya
 HATA ALA HII YA MUZIKI NAJUA KUITUMIA: Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kuungurumisha ngoma inayotumbuizwa kwa mtungi na kigoda, iliyokuwa ikipigwa na kina mama katika kijiji cha Udinde, Chunya
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano Udinde, Chunya
 Wananchi kwenye mkutano wa Kinana, Udinde: Imetayarishwa na theNkoromo Blog

ZIARA YA KINANA JIMBO LA SONGWE WILAYANI CHUNYA YAFANA, AFUNGUA NA KUSHIRIKI UJENZI WA MIRADI YA MAENDELEO

 KATIBU Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana akishiriki na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kati) na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano w... [Read More]