Google PlusRSS FeedEmail

JAMBO LEO, CAG AMEMRUKA VIPI NAPE?

Agosti 27, 2013, Chama Cha Mapinduzi kilitoa matamko kadhaa yaliyokuwa yamepitishwa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, Taifa mjini Dodoma. Baadhi ya mambo ambayo CCM kupitia kwa Katibu wake wa NEC, Irikadi na Uenezi Nape Nnauye iliyoyaeleza kwa waandishi wa Habari tena yakiwa yameandikwa kwenye karatasi ambazo baadaye waandishi hao walipewa, Kamati Kuu hiyo vilivyokuwa imelishughulikia suala la madiwani wanane wa CCM waliokuwa wamefukuzwa na Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Kagera kwa madai ya utovu wa nidhamu.

Miongoni mwa maamuzi waliyopewa waandishi wa habari ni kwamba, Kamati Kuu iliitaka serikali kumwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Seriali (GAC) kufanya ukaguzi maalum wa haraka wa mambo  yanayolalamikiwa dhidi ya Meya ili ukweli ujulikane na matokeo ya uchunguzi huo yawasilishwe kwenye Baraza la madiwani ili hatua stahiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria na taratibu zinazoongoza Serikali za mitaa.

Sasa mdau, soma habari hii hapo chini, kama ilivyoandikwa leo, Septemba 25, 2013,  katika ukurasa wa 6, gazeti la Jamboleo halafu utafakari kama kweli aliyeandika habari hii alielewa vema na kujiridhisha vya kutosha mantiki ya habari yake kabla ya kumpatia mhariri

Zipo hoja nyingi kwenye habari hii lakini MOJA: ni kwamba; Kama CAG anakiri kwamba ukaguzi huo unafanyika kwa ombi maalum lililotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, sasa hapo huyo CAG amemruka vipi Nape? (ingawa hata aliyekuwa ameagiza serikali kumtuma CAG si Nape ni Kamati Kuu ya CCM, ila Nape alikuwa msemji tu wa agizo).

PILI: Hivi ni hekima ya aina gani inayoweza kusadiki kwamba, agizo au hata ombi linalotolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwenda kwa CAG, halimhusu Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye bosi wa hao wote!

Vifuatavyo ni vipande vya habari hiyo na Press Release ya CCM inayoonyesha kwamba CCM (siyo Nape) iliiagiza serikali yake, kumtuma CAG.





This entry was posted in

Leave a Reply