Google PlusRSS FeedEmail

ZIARA YA KINANA WILAYANI CHUNYA MOTO, AMZOA KATIBU WA CHADEMA WA WILAYA HIYO, AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, WANANCHI WAFURIKA KWENYE MIKUTANO YAKE

 Aliyekuwa Katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, Bryson Mwasimba akionbyesha kadi yake ya chama hicho, kabla ya kumkabishi Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto), alipotangaza kuhamia CCM, leo jioni katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika Kata ya Lupa, wilayani humo.
 Bryson Mwasimba kutoka Chadema akikabishi kadi yake kwa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
 "Sasa Nataka kuungama dhambi nilizowafanyia ndugu zanguni wakati nikiwa Chadema, Niliwadanganya mengi nanyi mkaniamini. Sasa naungama kwenu mnisamehe, Lakini mjue kwamba wenye lawama kubwa ni Chadema kwa sera zao za kuhimiza wanachama na viongozi wake kuwa waongo. Sasa kabla sijaendelea kusema yaliyo safi naomba kwanza nilivue gwanda hili la Chadema maana linaninajisi", alisema Bryson, akiwa jukwaani baada ya kutangaza kuhamia CCM kwenye mkutano huo.
 "Sasa ngoja nilivulie mbali hili kwanda nibaki huru", akasema Bryson wakati akilivua  gwanga lake la Chadema, huku akiwa ameshikilia mdomoni kadi yake mpya ya CCM aliyokabidhiwa na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kushoto).
 Baada ya kulkivua gwanda, Bryson akavaa shati la kijani la CCM.
 Kisha akazungumza ya moyoni, huku akimtwisha mzigo wa Lawama Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu, kwamba amekuwa akimtumbukiza kwenye madeni mbalimbali kwa kutumia huduma kisha kusepa bila kulipa.  Wakati akisema hayo Nape alikuwa upande wa kulia akimtazama na kumsikiliza kwa makini sana
Ikawa nderemo na hoi hoi Bryson akabebwa na wana CCM kwa furaha

KABLA YA HAPO KINANA ALIKAGUA UJENZI BARABARA YA MBEYA-CHUNYA HADI TABORA INAYOJENGWA NA KAMPUNI YA CCCC YA CHINA
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na wasaidizi wake, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakikagua sehemu ya ujenzi wa barabara ya Mbeya-Chunya inayoenda hadi Tabora, unaofanywa na Kampuni ya Kichina ya CCCC, wakati Kinana na msafara wake walipokuwa wakipita katika eneo hilo, akiwa njiani kwenda wilayani Chunya, leo
 Baadhi ya maeneo yanajengwa kwa uhodari mkubwa kiasi kwamba kupita ni lazima kuruka, Hapa Katibu wa NEC, Itukadi na Uenezi akiruka kutoka upande mmoja kwenda mwingine wa eneo hilo linalojengwa.Nyuma yake ni Kinana ambaye naye alimfuata Nape pia kwa kuruka eneo hilo
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akiruka eneo hilo
Kazi ya kuopasuka milima na kuweka sawa inapopita barabara hiyo, ikiendelea

MIKUTANO NA SHUGHULI NYINGINE ZA KINANA WILAYANI CHUNYA
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Katibu wa NEC, Itukadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwaslimia wananchi, baada ya msafara wa Kinana kuwasili wilayani Chunya
 Kinana akiwasalimia wananchi baada ya kusimamia msafara wake akiwa njiani kwenda Chunya
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua shina la wakereketwa wajasiriamali wa CCM katika kituo cha mabasi mjini Chunya.
 Kisha akakabidhi kazi za CCM kwa wanachama wapya 100 kwenye shina hilo
 Kinana akihutubia baada ya kizindua shina hilo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsikiliza Kijana, Frank Mwapololo, ambaye ni mmoja wa wachimbaji wadogo katika machimbo ya mafunzo kwa ajili ya wachimbaji wadogo, yaliyopo Chunya, alipozungumza na wajasiriamali wa mradi huo, Nov 30, 2013, akiwa katika ziara kukagua utekelezaji wa ilani ya chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia sahihi ya kuzitatua, mkoani Mbeya.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (wapili kulia) akimrekebishia sawasawa vazi, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, baada ya wazee wa Kata ya Lupa, wilayani Chunya, kumvalisha vazi la wazee wa Kata hiyo, akiwa katika ziara kukagua utekelezaji wa ilani ya chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia sahihi ya kuzitatua, mkoani Mbeya
 Katibu Mkuu wa CCM akiwahutubia wananchi wa Kata ya Lupa,
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi mashine isiyotumia umeme, ya kufyatulia matofali, kwa kikundi cha wajasiamali, wakati wa mkutano wa hadhara aliofanya Nov 30, 2013, katika Kata ya Lupa, wilayani Chunya, akiwa katika ziara kukagua utekelezaji wa ilani ya chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia sahihi ya kuzitatua, mkoani Mbeya, Nov 30, 2013. Wengine ni Mkuu wa mkoa huo, Abbas Kandoro na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye. Imatayarishwa na theNkoromo Blog

This entry was posted in

Leave a Reply