Google PlusRSS FeedEmail

NAPE ALITEKA JIMBO LA UBUNGO ENEO LA KIMARA

*ASEMA CHADEMA SASA INAKUMBATIA UKAWA KUJARIBU KUPOZA MIGOGORO YA NDANI INAYOKIMALIZA.

*ATABIRI MAISHA YA  CHADEMA KUKOMA BAADA YA AJENDA YA KATIBA  MPYA KUMALIZIKA

*ASEMA, 'PANGO' LA MYIKA UBUNGO NALO MWISHO 2015

NA BASHIR NKOROMO, KIMARA
KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye,  leo ametoboa siri kwamba, viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema wamelazimika kukumbatia kinachoitwa Umoja wa Katiba ya wananchi (UKAWA), ili kujaribu kupoza migogoro iliyopo ndani ya chama hicho ambayo inakiua.

Amesema, siyo kweli kwamba Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Woilbrod Silaa na Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe wanahangaika na muungano huo unaoitwa wa kutafuta Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwa lengo la kusaidia wananchi bali ni kujaribu kupoza makali, baada ya kuona kwamba chama chao kimo katika mgogoro mkubwa wa ndani ambao si mda mrfu unakimaliza.

"Chadema wapo katika mgogoro mkubwa unaokitafuta kutokana na baadhi ya viongozi wake hasa wa ngazi za juu kukiendesha chama katika misingi ya ubaguzi.. na ndiyo sababu leo au hata kesho, Mbowe hawezi kuitisha kikao cha Baraza Kuu la chama hicho, na akijaribu kufanya hivyo anatimuliwa", alisema Nape.

Nape pia hakumuweka kiporo Mbunge wa jimbo la Ubungo, John Mwinyika, badala yake alimpasha kwenye mkutano huo kwamba, baada ya wananchi wa jimbo hilo kudanganyika na kumpa ubunge, sasa akae mkao wa kuondoka baada ya uchaguzi mkuu utakaofanyika 2014.

"Mnyika na Chadema yake tunawambia pango lao hapa jimbo la Ubungo  linamalizika rasmi mwaka 2014 na hatuma mpango wa kumuongezea, kilichobaki sasa ajiandae tu kuondoka taratibu", alisema Nape.

Alisema, Mnyika kama walivyo wabunge katika maeneo ambako wananchi walijaribu kuwachagua wapinzani, anachofanya yeye na Chama chake cha Chadema ni kupambana na kujenga misingi ya chama chao kuendelea kuwa kuishi na kamwe hawashughulikii matatizo ya wananchi.

"Na hili niliwaambia miaka mingi iliyopita, nilisema hapa ubungo kwamba mkimchagua mpinzani kazi yake itakuwa kutafuta njia za kuimarisha chama chake, na kamwe hataweza kujihusisha na masuala ya maendeleo yenu", alidai Nape na kuongeza;-

"Mnyika kama kweli una lengo la kuwatumikia wananchi wa Ubungo, umefika wakati wa kuacha sasa na mambo ya kudai kila mara hoja binafsi bungeni, sasa udai na hoja za wananchi, maana ukiendelea kudai hoja binafsi zaa wananchi utadai lini?"

Alisema, ni kutokana na wapinzani akiwemo Mnyika na chama chake cha Chadema, kutokwa mapovu midomoni kila kona ya nchi wakihangaika na Katiba mpya, tena wanachozungumzia zaidi serikalikali tatu na kusingizia kwamba ndiyo mahitaji ya wananchi huku wakijua wazi kwamba wanachohitaji wananchi kama wa Ubungo ni maji, elimu na afya na siyo idadi ya serikali.
 
Nape alisema hivi sasa wananchi wameshastukia vyama vya upinzani kwamba vipo kwa maslahi ya wachache ni si ya wananchi kama vinavyovyojinadi.

Alisema, miongoni mwa dalili za wananchi kuvistukia vyama cya upinzani, ni hali ilivyojitokeza wakati wa ziara za Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alkizofanya akiambatana na Nape mwenyewe mikoani.

Nape alisema, katika ziara hizo hadi sasa wanachama  12, 430 walijiunga CCM huku karibu nusu yao wakiwa wametoka katika vyama vya upinzani vikiwemo Chadema na CUF.

Katika mkutano huo ulioandaliliwa na Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Nape alipokea wanachama wapya 480, wengi wao wakiwa wamehamia CCM kutoka katika vyama vya Chadema na CUF kwa nyakati tofauti.
 Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Dar es Salaam, Ramadham Madabiba akimlaki Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape  Nnauye alipowasili katika Kata ya Kimara kwa ajili ya ziara ya siku moja kukagua uhai wa Chama katika kata hiyo, leo Juni 15, 2014.
Vijana wa Chipukizi wa CCM, wakimvisha skafu Nape alipowasili katika kata hiyo kuanza ziara ya siku moja leo,Juni 15, 2014. Kushoto ni Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Cholage na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge

Nape akizindua Shina la wakereketwa wacheza bao, tawi la Jumuia ya Wazazi la 770, Kimara, wakati wa ziara hiyo.
Nape akicheza bao na Augustine Bathoromew (66), baada ya kuzindua shina la wacheza bao la Jumuia ya Wazazi tawi la 770 Kimara akiwa katika ziara hiyo. Wanaoshuhudia ni Madenge (kulia) na katikati ni Madabiba na Juma Simba ambaye ni Katibu Mwenezi mkoa wa Dar es Salaam.
Nape akisalimia wananchi baada ya kuwasili uwanja wa mkutano wa Kimara TRA, kuhutubia mkutano wa hadhara mwishoni mwa ziara yake ya siku moja katika Kata ya Kimara.
Wananchi  wakimshangilia Nape baada ya kuwasili uwanja wa mkutano wa Kimara TRA
Wananchi wakiselebuka wakati Nape akicharaza gita na bendi ya Vijana Jazz, baada ya kuwasili uwanja wa mkutano wa Kimara TRA,wakati wa ziara hiyo.
Madabida akimkaribisha Nape kuhutubia kwenye mkutano huo
Nape akihutubia kwenye mkutano huo, mwishoni mwa ziara yake katika kata ya Kimara
Nape akimkabidhi kadi ya CCM, Domina Emmanuel, wakati wa mkutano wa hadhara Kimara TRA. Jumla ya wanachama wapya 480 wakiwemo waliohamia CCM wakitoka vyama vya Chadema na CUF walipewa kadi baada ya kujiunga na CCM
Nape akiongoza viongozi wengine kuwaunga mkono wanachama wapya kula kiapo baada ya kuwakabidhi kadi za CCM kwenye mkutano huo.
Wanachama waliopewa kadi kwenye mkutano huo, wakila kiapo.
Nape akiondoka baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara Uwanja wa Kimara TRA. Picha zote na Bashir Nkoromo-CCM Blog

This entry was posted in

Leave a Reply