Google PlusRSS FeedEmail

EWURA YAFURA LESENI ZA KAMPUNI KUBWA TISA ZA KUUZA MAFUTA

BODI ya Wakurugenzi  ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imefuta leseni za kufanya biashara ya mafuta kwa jumla (Whole Sale Licenses) kwa Kampuni tisa (9) zinazojihusisha na biashara hiyo hapa nchini. 
Uamzi huo umefanywa leo  (29.4.204) katika kikao chache cha Bodi ya Wakurugenzi kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa EWURA, Bw. Simon Sayore kutokana na kampuni hizo kukiuka masharti ya biashara.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Bw. Felix Ngamlagosi, kufutwa kwa leseni hizo kumetokana na ukikaji kwa sheria na kanuni za biashara hiyo.
Bw. Ngamlagosi katika taarifa yake, alisema kampuni hizo zimefutiwa leseni kutokana na kukaa bila kuagiza mafuta kama leseni inavyowataka kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita tangu kupewa leseni hizo na EWURA.

Kampuni zilizofutiwa leseni ni pamoja na Aspam Energy (T) Limited, MPS Oil Tanzania Limited, Panone Bulk Oil Importers Limited, Petcom (T) Limited, KMJ Tanzania Limited, Horizon Petroleum Company Limited, G.M and Company (T) Limited na Petronas Energy Tanzania Limited.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeundwa chini ya sheria ya EWURA, sura namba 414 ya Sheria za Tanzania. EWURA ina majukumu ya kusimamia shughuli za udhibiti, kiufundi na kiuchumi  katika  sekta Nne (4)  za Petroli, Umeme, Gasi Asili na Maji Safi na Maji Taka.

IMETOLEWA NA
BW. FELIX NGAMLAGOSI
MKURUGENZI MKUU
EWURA

This entry was posted in

Leave a Reply